Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 3 | Sitting 6 | Finance | Wizara ya Fedha | 53 | 2026-04-10 |
Name
Mabula Johnson Magangila
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Msalala
Primary Question
MHE. CHARLES M. NJAMA K.n.y. MHE. MABULA J. MAGANGILA aliuliza: -
Je, lini Serikali itaanza kutumia rasilimali zake kama dhamana, ili Wafanyabiashara wa Kitanzania waweze kukopesheka zaidi?
Name
Laurent Deogratius Luswetula
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kavuu
Answer
NAIBU WAZIRI WA FEDHA (MHE. LAURENT D. LUSWETULA) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Fedha, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mabula Johnson Magangila, Mbunge wa Jimbo la Msalala kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, Serikali ya Tanzania imefanya jitihada za kuwezesha upatikanaji wa mitaji kwa wafanyabiashara wawekezaji kwa kutumia rasilimali zake kama dhamana, kupitia mikopo yenye masharti nafuu inayotolewa kwa wafanyabiashara wadogo na wa kati kupitia Benki ya NMB kwa riba ya asilimia saba tu kwa mwaka. Hatua hii inalenga kuongeza uwezo wa kukopesheka na kukuza uchumi wa wananchi.
Mheshimiwa Spika, Serikali imeendelea na jitihada za kuwawezesha wananchi kiuchumi. Imeipatia Benki Kuu ya Tanzania wajibu wa kusimamia Mifuko ya Udhamini wa Mikopo, ambayo inatoa udhamini kwa Watanzania wenye miradi yenye tija katika sekta mbalimbali za uchumi, lakini wana changamoto za dhamana zinazohitajika wakati wa kuomba mkopo, ili waweze kupata mikopo kupitia taasisi za fedha.
Mheshimiwa Spika, wafanyabiashara wanaweza kunufaika na huduma za Mfuko wa Udhamini wa Mikopo ya Mauzo ya Nje ya Nchi (Export Credit Guarantee Scheme) huku wajasiriamali wadogo na wa kati wakinufaika kupitia Mfuko wa Udhamini wa Mikopo kwa Wajasiriamali Wadogo na wa Kati (Small and Medium Enterprises Credit Guarantee Scheme). Mfuko huu una lengo la kurahisisha upatikanaji wa mikopo, kukuza miradi ya kiuchumi na kuongeza tija katika sekta zote za uchumi.
Mheshimiwa Spika, ninaomba kuwasilisha.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved