Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Juliana Daniel Shonza
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. JULIANA D. SHONZA aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kuanza utekelezaji wa Mradi mkubwa wa Maji kutoka Mto Momba ili kuboresha huduma ya maji kwa wananchi?
Supplementary Question 1
MHE. JULIANA D. SHONZA: Mheshimiwa Spika, ninashukuru. Kwa kuwa, mradi huu ulizinduliwa mwezi Machi, 2025 na mpaka sasa ni mwaka mmoja kamili umepita bado tuko kwenye hatua za awali. Kwenye majibu ya msingi Mheshimiwa Waziri amesema kwamba mradi unatarajiwa kukamilika mwaka mmoja na nusu tu kutoka sasa.
Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Waziri, haoni sasa kuna haja kubwa ya Serikali kuanza kuongeza kasi ya utoaji fedha, na vilevile usimamizi, ili mradi huu uweze kukamilika kwa wakati, ikizingatiwa kwamba, wanawake wenzangu wa Mji wa Tunduma, Mji wa Mlowo pamoja na Mji wa Vwawa wanapata shida kubwa sana ya maji? Ahsante. (Makofi)
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ninapenda kumpongeza Mheshimiwa Juliana Daniel Shonza, Mbunge wa Viti Maalumu, kwa swali lake. Ni kweli kabisa Mheshimiwa amekuwa sehemu ya utafutaji wa miradi ya maendeleo ndani ya Mkoa wa Songwe na amekuwa akishirikiana vizuri kabisa na Waheshimiwa Wabunge wenzake wa majimbo. Pia, tunatambua kwamba, mradi huu ambao ni uwekezaji mkubwa sana wa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, zaidi ya shilingi bilioni 119 zimewekezwa pale.
Mheshimiwa Spika, pia, tunafahamu kwamba, mkandarasi alikuwa anahitaji advance ya zaidi ya shilingi bilioni 17. Hivi sasa tayari tumemlipa shilingi bilioni 5.9 na tunaendelea na hatua nyingine za kumalizia ile fedha iliyobaki. Tayari tumefanya site possession, tarehe 18 mwezi wa Tatu, yuko site, mradi umeanza na uko katika asilimia moja nukta saba.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, ninamtoa hofu Mheshimiwa Mbunge, Serikali dhamira yake ni kuhakikisha kwamba, mradi huu unaenda kuendelea vizuri na ukamilike kwa wakati. Pale tutakapoona inabidi, huwa tunatoa maelekezo kwa wakandarasi kuongeza wafayakazi na kufanya kazi usiku na mchana. Lengo ni kwamba, ukamilike ndani ya muda wa mkataba. Ninashukuru sana. (Makofi)
Name
Joshua Samwel Nassari
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Arumeru-Mashariki
Primary Question
MHE. JULIANA D. SHONZA aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kuanza utekelezaji wa Mradi mkubwa wa Maji kutoka Mto Momba ili kuboresha huduma ya maji kwa wananchi?
Supplementary Question 2
MHE. JOSHUA S. NASSARI: Mheshimiwa Spika, ninashukuru kwa kuniona na mimi niulize swali dogo la nyongeza kwa Waziri wa Maji hapo. Kuna miradi mingi ya maji pale Arumeru, ambayo Serikali imeiasisi, lakini miradi ile imesimama kwa sababu ya kukosa fedha. Mathalani Mradi wa Imbaseni, Maji ya Chai, Kikatiti mpaka Maroroni, halikadhalika Mradi wa kule Uwiro, yote imesimama kwa sababu, certificates hazijalipwa. Je, Serikali inatoa commitment gani, ili wakandarasi waweze kurudi site?
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Nassari, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, kwanza pamoja na kuuliza swali, Mheshimiwa Nassari tumekuwa tukizungumza sana mara kwa mara kuhusiana na suala hili. Kuna kipindi tulipanga ziara ya kwenda kuona namna gani tunaweza tukachukua hatua, ili miradi hii iweze kukamilika; lakini nimtoe hofu, miradi na wakandarasi wake tumeanza kufanya engagement, ili kuona namna gani tunakubaliana wakati tunashughulika kuhusu malipo ya hati zao za madai. Wao warudi site, ili kuhakikisha tusiwe na gap lolote hapa Katikati. Lengo ni kwamba, mradi ukamilike kwa wakati, na fedha zao waweze kulipwa wasije wakawa na changmoto yoyote ya kifedha. Ninakushukuru sana.
Name
Subira Khamis Mgalu
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. JULIANA D. SHONZA aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kuanza utekelezaji wa Mradi mkubwa wa Maji kutoka Mto Momba ili kuboresha huduma ya maji kwa wananchi?
Supplementary Question 3
MHE. SUBIRA K. MGALU: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza. Kwa kuwa, Kata za Fukayosi na Makurunge, Jimbo la Bagamoyo, zina changamoto kubwa ya maji kwa vile tu zimeunganishwa na miundombinu ya maji kutoka Mto Wami, ilhali wapo karibu na chanzo cha maji cha Mto Ruvu Chini na mara kadhaa kumekuwa na ahadi ya kuwaunganisha sasa na miundombinu ya maji kutoka Ruvu Chini, je, wananchi hawa wawe na matumaini na mwaka wa fedha 2026/2027 kwamba, ahadi hiyo itatimizwa? Ahsante. (Makofi)
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ninapenda kujibu swali dogo la Mheshimiwa Subira Mgalu, Mbunge wa Bagamoyo. Bahati nzuri ni kwamba, mradi ambao unaenda kutatua changamoto ya wananchi wa Bagamoyo, na kwa vile ameuliza matumaini, ni kweli kabisa wananchi wawe na matumaini katika mwaka 2026/2027; tunaenda kuwaingiza kwenye bajeti hiyo ili waweze kufikishiwa huduma ya majisafi na salama.
Mheshimiwa Spika, kikubwa tu ni kwamba, tuendelee kuwa na subira kwa sababu, miradi iko mingi ambayo bado iko kwenye utekelezaji; zaidi ya miradi 200 na kitu kwa mijini, na ni zaidi ya miradi 878 ambayo ina gharama ya shilingi trilioni 1.3. Bado tutahitaji kuanzisha miradi ambayo itakuwa ya kimkakati, ikiwemo ndani ya Jimbo la Bagamoyo. Ninakushukuru sana.

Supplementary Question 4

Supplementary Question 5

Supplementary Question 6