Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 3 | Sitting 6 | Water and Irrigation | Wizara ya Maji | 51 | 2026-04-10 |
Name
Juliana Daniel Shonza
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. JULIANA D. SHONZA aliuliza:-
Je, Serikali ina mpango gani wa kuanza utekelezaji wa Mradi mkubwa wa Maji kutoka Mto Momba ili kuboresha huduma ya maji kwa wananchi?
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-
Mheshimiwa Spika, Serikali imeanza utekelezaji wa mradi mkubwa wa kutoa maji Mto Momba kwenda miji ya Vwawa, Mlowo na Tunduma kwa gharama ya shilingi bilioni 119.95. Miongoni mwa kazi zinazotekelezwa kupitia mradi huo ni pamoja na ujenzi wa chanzo cha maji chenye uwezo wa kuzalisha maji lita milioni 21.5 kwa siku.
Mheshimiwa Spika, ujenzi wa mtambo wa kuchuja na kutibu maji (treatment plant) chenye uwezo wa kutibu maji lita milioni 20 kwa siku, ujenzi wa matanki matatu yenye jumla ya ujazo wa lita milioni 10 sanjari na ulazaji wa mabomba umbali wa kilometa 317.
Mheshimiwa Spika, mradi huo upo kwenye hatua za awali za utekelezaji ambapo unatarajiwa kukamilika mwezi Septemba, 2027 na kunufaisha zaidi ya wananchi 1,245,000 wa miji ya Tunduma, Vwawa, Mlowo pamoja na vijiji 31 vya Wilaya ya Momba.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved