Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Najma Murtaza Giga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. NAJMA MURTAZA GIGA K.n.y. MHE. MECKTRIDIS F. MDAKU aliuliza:- Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa barabara ya kutoka Ifakara – Lupilo hadi Malinyi kwa kiwango cha lami?

Supplementary Question 1

MHE. NAJMA MURTAZA GIGA: Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Wanamalinyi, ninaishukuru sana Serikali kwa majibu yenye kuleta matumaini. Nina swali moja la nyongeza. Barabara ya Malinyi - Natumbo ni barabara mtambuka na inaweza kuunganisha mikoa zaidi ya miwili. Je, Serikali itatimiza lini ahadi yake ambayo imeitoa kwa muda mrefu?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba hiyo barabara inaunganisha Mkoa wa Morogoro na Mkoa wa Ruvuma na ni barabara kuu. Awali tulitakiwa tujenge barabara yote hiyo, lakini kwa sababu za kibajeti ndiyo maana tumeanza kuigawa kwa vipande.

Mheshimiwa Spika, kwa awamu ya kwanza tutajenga kilometa 112, na tumesema kwenye jibu la msingi, tayari tumeshasaini hata mkataba na huyo mkandarasi. Kilichobaki sasa ni kumlipa fedha ya awali ili aanze kuijenga hiyo barabara kilometa 112, na baada ya hapo mpango ni kukamilisha hadi Mkoa wa Ruvuma pale Songea, ahsante.

Name

Devotha Daniel Mburarugaba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. NAJMA MURTAZA GIGA K.n.y. MHE. MECKTRIDIS F. MDAKU aliuliza:- Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa barabara ya kutoka Ifakara – Lupilo hadi Malinyi kwa kiwango cha lami?

Supplementary Question 2

MHE. DEVOTHA D. MBURARUGABA: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi. Kwa maslahi mapana ya wananchi wa Mkoa wa Kagera, ni lini Barabara ya Nyakahura – Rulenge - Murugarama itajengwa kwa kiwango cha lami? Tunafahamu barabara hiyo ina kilometa 141 na ni barabara ya kimkakati ndani ya Wilaya ya Ngara.

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba barabara aliyoitaja kwanza tunaitambua, ndiyo barabara ambayo inaenda kwenye machimbo ya Nikeli. Kwa hiyo, kama Serikali ninapenda umhakikisha Mheshimiwa Mbunge na wananchi wa Ngara kwamba Barabara ya Nyakahura, Muguga, Rulenge hadi Ngara yenyewe, ipo kwenye mpango.

Mheshimiwa Spika, ninamhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba mtupitishe bajeti kwa sababu iko kwenye mpango wa kuanza kuijenga kwa kiwango cha lami. Ninadhani ataiona kwenye bajeti yetu siku tutakapokuwa tunaisoma hapa, ahsante.

Name

Tinnar Andrew Chenge

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. NAJMA MURTAZA GIGA K.n.y. MHE. MECKTRIDIS F. MDAKU aliuliza:- Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa barabara ya kutoka Ifakara – Lupilo hadi Malinyi kwa kiwango cha lami?

Supplementary Question 3

MHE. TINNAR A. CHENGE: Mheshimiwa Spika, kwa kuwa ni sera ya Serikali kuhakikisha kwamba kila makao makuu ya mkoa yanaunganishwa na mikoa jirani kwa barabara za lami. Je, ni lini Serikali itaanza kujenga kwa kiwango cha lami barabara ya kutoka Bariadi na Gangabilili – Mwanhuzi – Sibiti - Iguguno na Singida? Ahsante.

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, hili swali linafanana na swali la msingi kwa sababu ndiyo barabara ambazo zinatakiwa zijengwe zote. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba kwa sasa kwa awamu hii tumepanga kujenga kiwango cha lami kilometa 50 katika hiyo barabara ya Bariadi – Sibiti kuja Singida.

Mheshimiwa Spika, tayari tuna mkandarasi, na tunachosubiri ni kulipa malipo ya awali ikiwa ni pamoja na kujenga barabara kwa kiwango cha lami katika lile daraja la Sibiti ambapo kutakuwa na upande wa Sibiti kwa maana ya Simiyu na upande wa Singida, ahsante.