Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Masache Njelu Kasaka

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Lupa

Primary Question

MHE. MASACHE N. KASAKA aliuliza:- Je, lini ujenzi wa Mradi wa Maji Chunya uliosainiwa na kutengewa fedha utaanza ?

Supplementary Question 1

MHE. MASACHE N. KASAKA: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu ya Serikali ambayo imeweza kuyatoa, lakini wananchi wa Chunya wamenituma maji. Kwa kuwa Serikali inaendelea kutafuta fedha ili kuweza kutekeleza mradi huu ambao utekelezaji wake utachukua zaidi ya miaka miwili, je, kwa nini sasa Serikali isianze kutekeleza mradi huu kwa kiasi cha fedha kilichokuwepo (dola milioni sita) ambazo takribani ni zaidi ya shilingi bilioni 13 ili kuanza hatua za mwanzo, kwa maana ya kwenye chanzo, pamoja na tenki na power house, ili fedha nyingine zinazopatikana utekelezaji wake uweze kukamilika? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili, kwa kuwa mji wa Chunya Mjini una changamoto kubwa sana ya maji na mradi huu utekelezaji wake utachukua muda mrefu, je, ni upi mpango wa Serikali wa muda mfupi wa kuchimba visima vichache ili viweze kushirikiana na vilivyokuwepo ili changamoto ya maji Chunya Mjini iweze kutatulika?

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, kwa dhati kabisa ninampongeza Mheshimiwa Masache ambaye amekuwa sauti imara ya Wananchi wa Lupa hasa katika kuwatetea na kuhakikisha kwamba huduma ya majisafi na salama inaendelea kuimarishwa.

Mheshimiwa Spika, kwenye suala la kwanza nimtoe hofu kwamba Serikali baada ya kubaini kwamba visima vile havina ubora unaotakiwa kupeleka maji kwa wananchi, lakini pia visima vile havina uwingi wa maji kulingana na usanifu wa mahitaji halisi ya eneo husika, tukabaini kuna chanzo kingine.

Mheshimiwa Spika, maana yake ni kwamba scope ya kazi ikabadilika na gharama zake zikabadilika, lakini kwa sababu fedha hizi ziko committed kwa ajili ya kutekeza mradi huo, hatuwezi kuanza kuzitumia kabla ya makubaliano na Serikali iliyotoa hizo fedha kuhakikisha kwamba tuwe na maelewano ili watoe kibali kama ni kuendelea ama tusubiri ili waongeze fedha ili tukatekeleze na kufanya shughuli zote kwa pamoja bila kuwa na changamoto.

Mheshimiwa Spika, ninamwomba Mheshimiwa Mbunge awe na subira katika hili kwa niaba ya wananchi wake wa Lupa, tunamhakikisha Serikali tuko makini na tunaendelea na mchakato huo na tuko katika hatua nzuri kabisa.

Mheshimiwa Spika, katika eneo lingine kwa swali la pili ni kuhusiana na kwamba tufanye juhudi za dharura; Mheshimiwa Mbunge ni shahidi, kwanza kabisa tunavyo visima vitatu pale ambavyo vimechimbwa na vinatoa maji takribani lita 692,000 kwa siku.

Mheshimiwa Spika, pia Serikali kupitia Wizara ya Maji kwa kutumia wataalamu wetu wa ndani na kutumia mitambo ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyoinunua, tumechimba pale kisima ambacho sasa kinatoa lita 412,000 kwa siku ambapo tunaamini kwamba kutoka kwenye mahitaji ya milioni 4.3 tukajumlisha 692,000, tukajumlisha 412,000 mahitaji yetu yanazidi kupungua, na sasa upatikanaji wa maji unaenda kuwa zaidi ya 56% kwa Mji wa Lupa.
Mheshimiwa Spika, nimtoe hofu Mheshimiwa Mbunge, tuko makini na tumejizatiti kwenda kutatua huduma ya majisafi na salama katika Mji wa Lupa.

Name

Ritta Enespher Kabati

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MASACHE N. KASAKA aliuliza:- Je, lini ujenzi wa Mradi wa Maji Chunya uliosainiwa na kutengewa fedha utaanza ?

Supplementary Question 2

MHE. DKT. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi niulize swali dogo la nyongeza. Kata ya Mahenge katika Jimbo la Kilolo lina chanzo kizuri sana cha maji na tayari Serikali ilishafanya upembuzi yakinifu. Je, ni lini sasa watapatiwa mradi wa maji ili wananchi waweze kupata majisafi na salama?

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ni kweli kabisa Serikali inaendelea kutekeleza miradi mbalimbali nchini, lakini cha kwanza kabisa ni kufanya mapitio ya mahitaji ya maji na baadaye tunafanya upembuzi yakinifu. Baada ya kufanya upembuzi yakinifu tunafanya usanifu wa kina ili ku-establish gharama za mradi unaoenda kutekelezwa.

Mheshimiwa Spika, nimtoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwa sababu upembuzi yakinifu umeshakamilika na sasa tunaandaa kwenda kufanya usanifu wa kina ili tuweze kupata gharama za mradi ili tuende kutekeleza na wananchi wake wa Jimbo la Kilolo wapate huduma ya majisafi na salama kutoka kwenye chanzo cha uhakika ambacho Mheshimiwa Mbunge amekigusia.