Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 3 | Sitting 13 | Water and Irrigation | Wizara ya Maji | 152 | 2026-04-21 |
Name
Masache Njelu Kasaka
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Lupa
Primary Question
MHE. MASACHE N. KASAKA aliuliza:-
Je, lini ujenzi wa Mradi wa Maji Chunya uliosainiwa na kutengewa fedha utaanza ?
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -
Mheshimiwa Spika, ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Masache Njelu Kasaka, Mbunge wa Jimbo la Lupa, kama ifuatavyo :-
Mheshimiwa Spika, Serikali ilisaini Mkataba wa ujenzi wa mradi wa maji kwa Mji wa Chunya mwezi Juni, 2022 ambapo ulikuwa ukitekelezwa kwa kushirikiana na Serikali ya India kwa gharama ya Dola za Marekani Milioni 6.59. Pamoja na kazi nyingine, Serikali ilipanga kuchimba jumla ya visima saba kama chanzo cha maji ambapo baada ya uchimbaji wa visima vya majaribio kufanyika ilionekana havikuwa na matokeo mazuri ya wingi na ubora wa maji unaokubalika kwa matumizi ya binadamu na mifugo.
Mheshimiwa Spika, matokeo hayo yalipelekea Serikali kutafuta chanzo cha maji mbadala ambacho ni Mto Gwaziva ambapo baada ya usanifu wa marejeo, sasa mradi huo unatarajiwa kugharimu jumla ya Dola za Marekani milioni 16 badala ya Dola za Marekani milioni 6.59 za awali.
Mheshimiwa Spika, kwa sasa Serikali inaendelea kutafuta fedha za utekelezaji wa mradi huo ikiwemo majadiliano ya kina na Serikali ya India ili kuhakikisha utekelezaji wa mradi huo unaanza katika mwaka wa fedha 2026/2027.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved