Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Benjamin Lukubha Ngayiwa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kahama Mjini

Primary Question

MHE. BENJAMIN L. NGAYIWA aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kukamilisha ujenzi wa chujio la maji la Buzwagi na tenki la maji la Shunu/Lugela ili kupunguza kero ya kukatika kwa maji Kahama?

Supplementary Question 1

MHE. BENJAMIN L. NGAYIWA: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri sana ya Wizara, ninaomba sasa nipate uhakika wa Mheshimiwa Naibu Waziri kwamba, je, yuko tayari kuambatana na mimi kwenye uzinduzi wa miradi hii ambayo amesema itakamilika mwezi Juni pamoja na kutembelea miradi mingine ya Kilago na Mondo ili kuwapatia wananchi wetu huduma ya maji?

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, kwanza ninampongeza sana Mheshimiwa Lukubha kwa kazi nzuri na kuwa sauti imara ya Wanakahama Mjini kwa kuendelea kuwatetea na hasa katika sekta yetu ya maji.

Mheshimiwa Spika, Serikali dhamira yake ni kuendelea kushirikiana na Wabunge wote. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, Serikali kupitia Wizara ya Maji, tuko tayari kuambatana naye kwenda kukagua utekelezaji wa miradi; pili, kuhakikisha ubora wa mradi uliokamilika; tatu, kuangalia thamani halisi ya mradi uliotekelezwa. Baada ya hapo uzinduzi wa miradi utatokea katika jimbo lake.

Mheshimiwa Spika, sisi Serikali hasa Wizara ya Maji tutaendelea kushirikiana naye.

Name

Cornel Lucas Magembe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chato Kaskazini

Primary Question

MHE. BENJAMIN L. NGAYIWA aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kukamilisha ujenzi wa chujio la maji la Buzwagi na tenki la maji la Shunu/Lugela ili kupunguza kero ya kukatika kwa maji Kahama?

Supplementary Question 2

MHE. CORNEL L. MAGEMBE: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru sana kupata nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Ninapenda kujua kutoka kwa Mheshimiwa Naibu Waziri kwamba mradi mkubwa wa maji uliojengwa kwenye Mji wa Chato ambao ni miongoni mwa miradi ya maji katika miji 28 sasa umekaribia kukamilika kwa 90%, lakini mpaka sasa sijaona kama hatua ya upelekaji maji imeanza. Katika vile vijiji 23 ambavyo mradi mkubwa umepita, vinavyotoka katika kata za Vikome, Ijamchele, Katende na Muungano, je, kauli ya Serikali ni nini juu ya mradi huo?

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ni kweli kabisa Serikali inaendelea kutekeleza mradi wa miji 28 katika Mji wa Chato, na kweli uko katika hatua nzuri kabisa, lakini sera yetu ya maji ni kuhakikisha kwamba pale ambapo chanzo cha maji kinatoka, wananchi wa eneo hilo wanakuwa wanufaika namba moja. Hilo la kwanza; pili, pale ambapo bomba kuu (transmission line) inapopita, wananchi left and right kilometa 12 wawe wanufaika wa maji ambayo yanachukuliwa kutoka kwenye chanzo; na tatu, kule sasa kulikokusudiwa kupeleka maji ndipo sasa watakuwa walengwa namba tatu.

Mheshimiwa Spika, hili tutaendelea kulisimamia isipokuwa kuna miradi ambayo tunaanza kwanza kwa kujenga bomba kuu, na baadaye zinaanza kupatikana offtake kulingana na vijiji sasa ambavyo vimepitiwa katika lile bomba kuu.

Mheshimiwa Spika, nimtoe hofu kwamba vijiji vyake tutahakikisha tunafanya usanifu na kufanya ile needs assessment ili kuhakikisha wananchi wa vijiji na kata ambazo Mheshimiwa Mbunge amezitaja, zinapitiwa na kunufaika na mradi huo wa maji kutoka miji 28.

Name

Issa Ally Mchungahela

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Lulindi

Primary Question

MHE. BENJAMIN L. NGAYIWA aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kukamilisha ujenzi wa chujio la maji la Buzwagi na tenki la maji la Shunu/Lugela ili kupunguza kero ya kukatika kwa maji Kahama?

Supplementary Question 3

MHE. ISSA A. MCHUNGAHELA: Mheshimiwa Spika, Mradi wa Mbangala umekuwa ukiahidiwa maji au utekelezaji wake kwa miaka mitatu mfululizo, na miongoni mwa watu ambao waliahidi ni yeye mwenyewe Naibu Naibu Waziri na tulikwenda naye mpaka kule kwenye kijiji cha Lupaso. Ni lini mradi huu utaanza kutekelezwa?

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ni kweli kabisa niliongozana na Mheshimiwa Mchungahela, tukaenda mwaka 2024, tulifika katika jimbo lake na hasa katika mradi huu wa Mbangala.

Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba mradi huu haujaanza kutekelezwa, lakini nimwahidi Mheshimiwa Mbunge kwamba bajeti ya 2026/2027 mradi huu tunahakikisha kwamba unakuwa kipaumbele ili sasa wananchi wa Mbangala waweze kwenda kupata huduma ya majisafi na salama.

Mheshimiwa Spika, nikiri kwamba tunayo miradi mingi inayoendelea, lakini kila mradi Serikali iko makini na imejizatiti kuhakikisha kwamba itachukua hatua kila fedha inapokuwa inapatikana. Lengo ni kwamba uwekezaji huu ukalenge kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya majisafi na salama.