Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Thomas Maganga Kampala

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Katavi

Primary Question

MHE. THOMAS K. MAGANGA aliuliza: - Je, lini Serikali itakamilisha malipo ya mkandarasi wa Mradi wa Bwawa la Nsekwa ili akamilishe kazi hiyo?

Supplementary Question 1

MHE. THOMAS K. MAGANGA: Mheshimiwa Spika, ninashukuru kwa majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri. Kwa mujibu wa mkataba wa mradi huo, mkataba unatarajiwa kukamilika Juni. Kwa majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri, mpaka sasa mradi uko 10%, je, Serikali ina kauli gani?

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, kwanza ninampongeza kwa ufuatiliaji wa karibu sana wa utekelezaji wa mradi huu; na pili, nimtoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwa sababu utekelezaji huu unaenda sambasamba na kukagua huu mradi mara kwa mara.

Mheshimiwa Spika, mradi huu ulichelewa kwa sababu ya changamoto ya kifedha, na sasa Serikali imeshatatua changamoto hiyo. Baada ya kuwa wamepelekewa fedha, wakandarasi wameanza kwa kasi kubwa.

Mheshimiwa Spika, tutatendelea kufuatilia kwa ukaribu sana, na vyombo vyetu vya usimamizi viko kule vinasimamia vizuri, wataalamu wetu, watendaji wakuu, Mheshimiwa Waziri pia anaendelea kuhakikisha kwamba mradi huu unakamilika kwa wakati na wenye thamani halisi ya fedha, kwa kuhakikisha kwamba ubora wake uendane na mahitaji halisi ili wananchi wa Jimbo la Mheshimiwa Kampala wapate huduma ya maji iliyokusudiwa.

Name

Mwantumu Mzamili Zodo

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. THOMAS K. MAGANGA aliuliza: - Je, lini Serikali itakamilisha malipo ya mkandarasi wa Mradi wa Bwawa la Nsekwa ili akamilishe kazi hiyo?

Supplementary Question 2

MHE. MWANTUMU M. ZODO: Mheshimiwa Spika, tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais kwa ujenzi wa Bwawa hili la Kwenkambala katika Jimbo la Handeni Mjini, ambao umekamilika katika hii Awamu ya Kwanza. Je, ni lini sasa Serikali itajenga chujio na kupandisha maji kwenye tenki kwa ajili ya wananchi kuendelea sasa kutumia maji haya? Ahsante.

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ninapenda kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Zodo. Kwanza ninampongeza sana kwa kazi nzuri anayoifanya kwa akina mama, hasa wa Mkoa wa Tanga. Ninampongeza kwa sababu amekuwa karibu sana na Wizara ya Maji kwa kushirikiana kutoa taarifa.

Mheshimiwa Spika, tunapochimba bwawa ama tunapokamilisha bwawa, kazi inayofuatia ni kuhakikisha kwamba tunajua queue ile ya maji ili tuweze sasa kufanya usanifu wa mtandao ambao utaenda kuhudumia wananchi.

Mheshimiwa Spika, nimtoe hofu, Serikali itapeleka fedha kwa ajili ya usanifu wa kuhakikisha kwamba unajenga tenki ili maji yaanze sasa kupelekwa kwa wananchi kama ilivyokusudiwa, ili wananchi wapate huduma ya majisafi na salama.

Name

Fagason Aron Nkingwa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbogwe

Primary Question

MHE. THOMAS K. MAGANGA aliuliza: - Je, lini Serikali itakamilisha malipo ya mkandarasi wa Mradi wa Bwawa la Nsekwa ili akamilishe kazi hiyo?

Supplementary Question 3

MHE. FAGASON A. NKINGWA: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi na mimi niweze kuuliza swali dogo. Jimbo langu la Mbogwe linazo kata 17, vijiji 87, vitongoji 335, lakini wananchi hawa hawana majisafi na salama. Je, ni lini Serikali italeta maji kwenye Jimbo langu la Mbogwe kutoka Ziwa Victoria?

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, labda niweke takwimu sahihi kwamba, siyo kwamba Jimbo la Mbogwe hakuna majisafi na salama. Tunafahamu kwamba mpaka sasa tuna zaidi ya 69% ya wananchi wa Mbogwe wanaopata huduma ya maji safi na salama. Nimtoe hofu, tunayo miradi inayoendelea ndani ya Jimbo la Mbogwe. Tutahakikisha kwamba tunaisimamia na tunapeleka fedha wakandarasi waweze kukamilisha miradi hiyo.
Mheshimiwa Spika, pia hatutamsahau katika maji kutoka Ziwa Victoria kwa sababu yeye yuko katika njia ambayo inaenda katika maeno ya Bukombe pamoja na Kahama. Hivyo, tunamhakikishia Mheshimiwa Mbunge kuwa wananchi wake wa Mbogwe watapata maji kutoka Ziwa Victoria bila ya kuwa na shida yoyote.

Name

Moshi Selemani Kakoso

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tanganyika

Primary Question

MHE. THOMAS K. MAGANGA aliuliza: - Je, lini Serikali itakamilisha malipo ya mkandarasi wa Mradi wa Bwawa la Nsekwa ili akamilishe kazi hiyo?

Supplementary Question 4

MHE. MOSHI S. KAKOSO: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi. Serikali iliahidi kuanza ujenzi wa kuleta maji kutoa Ziwa Tanganyika kuyaleta Mpanda Mjini. Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi huo ili wananchi waweze kunufaika?

SPIKA: Mheshimiwa Waziri.

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, kama sijamsikia vizuri kwenye hilo.

SPIKA: Unaweza ukarudia tena Mheshimiwa Kakoso swali lako?

MHE. MOSHI S. KAKOSO: Mheshimiwa Spika, Serikali iliahidi kuleta maji kutoka Ziwa Tanganyika kuyaleta Makao Makuu ya Mkoa wa Katavi Mpanda Mjini. Je, ni lini Serikali itaanza kutekeleza mradi huo?

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, katika mpango mahususi wa ujenzi wa gridi ya Taifa ya maji, moja ya maziwa na vyanzo vya uhakika ni pamoja na Ziwa Tanganyika, Ziwa Victoria, Ziwa Nyasa, pamoja na mito mingine mikubwa mikubwa kama Malagarasi, Momba, Pangani na mingineyo. Lengo la Serikali ni kuhakikisha kwamba maji tunayatumia kwa kuyapeleka katika makazi ya wananchi.

Mheshimiwa Spika, nimtoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali tayari imeshampata mtaalamu mshauri kwa ajili ya kuanza kufanya feasibility study ya kuyatumia maji ya kutoka Ziwa Tangayika ili yaende Kigoma, Mpanda, mpaka Rukwa. Lengo ni kuhakikisha kwamba wananchi wote wanaunganishwa na huduma ya maji yenye vyanzo vya uhakika, likiwemo Ziwa Tanganyika. Nakushukuru sana.