Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Yohana Stephen Msita

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Itigi

Primary Question

MHE. YOHANA S. MSITA aliuliza: - Je, upi mpango wa Serikali wa kuondoa kero ya wanyama waharibifu kama tembo kwenye Jimbo la Itigi?

Supplementary Question 1

MHE. YOHANA S. MSITA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali madogo ya nyongeza. Kwanza ninamshukuru sana Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu mazuri ya swali langu. Naomba kuuliza kwamba, kwa kuwa athari ni kubwa katika Vijiji vya Doroto, Kitaraka, Kihanju, Sanjaranda, Gurungu, Njirii, Aghondi, Kamenyanga, Kashangu na Idodyandole; na kulingana na majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri ni kwamba wamevuna tembo wawili: -

(a) Je, Serikali haioni sasa iko haja ya kuendelea kuvuna angalau hata tembo 20 ili kupunguza adha kwa wananchi kwa sababu athari ni kubwa sana?

(b) Je, Mheshimiwa Naibu Waziri atakuwa tayari kuambatana pamoja na mimi ili kwenda kujionea hali halisi ya athari iliyopo Jimbo la Itigi?

Name

Hamad Hassan Chande

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kojani

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, kwanza ninampongeza sana Mheshimiwa Yohana, kwani sasa amekuwa ni sehemu ya hifadhi, na pia anakuwepo ofisini mara kwa mara kutetea wananchi wake kwa usumbufu ambao wanaupata kutokana na wanyamapori hawa wakali na waharibifu.

Mheshimiwa Spika, ni kweli alichosema, kwamba Serikali imewahi kuvuna tembo wawili; na nimeona na nimesikia pendekezo lake kwamba tuendelee kuvuna, lakini kuvuna wanyama hawa ni lazima tufuate sheria, kanuni na taratibu. Kwa hiyo, tutaangalia taratibu, zikiruhusu, basi wale wanyama ambao wamekuwa ni wakali sana na ni waharibifu, inawezekana.

Mheshimiwa Spika, kwa swali lake la pili, mimi niko tayari kabisa kufuatana na ndugu yangu ili twende jimboni, tuone kadhia hiyo ili tuhami wananchi wetu, waweze kuendelea kuishi kwa tabasamu.

Name

Johannes Lembulung’ Lukumay

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Arumeru-Magharibi

Primary Question

MHE. YOHANA S. MSITA aliuliza: - Je, upi mpango wa Serikali wa kuondoa kero ya wanyama waharibifu kama tembo kwenye Jimbo la Itigi?

Supplementary Question 2

MHE. DKT. JOHANNES L. LUKUMAY: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi. Kwanza nichukue nafasi hii kumshukuru Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kulipa shilingi milioni 5.9 kwa wananchi 26 wa Kata za Kisongo, Musa na Mwandet ambao wameathiriwa na wanyamapori wakali sana.
Mheshimiwa Spika, wanyama hawa wamebadili tabia, wakawa wanashambulia watu na wahifadhi. Pia kuna majangili wanatumia silaha za kisasa, wanawashambulia wananchi na wahifadhi wa maliasili. Je, lini Serikali itawapatia wahifadhi wa maliasili waliopo Jimbo la Arumeru Magharibi silaha sitahiki aina ya SMG au AK-47 ili wahifadhi waweze kuokoa maisha ya wananchi na mali zao; pia wahifadhi wawalinde wanyamapori wetu ili wasiendelee kuuawa na hawa majangiri?

Name

Hamad Hassan Chande

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kojani

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Mbunge anataka kujua ni lini watapewa silaha hizo? Kwa mujibu wa sheria na kanuni zetu, wahifadhi wetu wana viwango maalumu vya umiliki wa silaha. Siyo kila aina ya silaha wanaweza kutumia.

Mheshimiwa Spika, ninachotaka kumhakikishia ni kwamba, Askari wetu wa hifadhi wataendelea kupewa silaha zinazostahiki kwao ili kuhami wanyamapori wetu na kupamba na majangili.

Name

Yahya Ally Mhata

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nanyumbu

Primary Question

MHE. YOHANA S. MSITA aliuliza: - Je, upi mpango wa Serikali wa kuondoa kero ya wanyama waharibifu kama tembo kwenye Jimbo la Itigi?

Supplementary Question 3

MHE. YAHYA A. MHATA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Moja ya kero kubwa, ndani ya Jimbo la Nanyumbu ni ongezeko la wanyama waharibifu, hasa tembo. Mheshimiwa Rais alipokuja wakati wa kampeni aliahidi kufungua kituo pale ndani ya jimbo langu, kwa maana ya kuongeza Askari na kutupatia ndege nyuki. Je, ni lini agizo hili la Serikali litatekelezwa ndani ya jimbo langu?

Name

Hamad Hassan Chande

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kojani

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, kwanza ninampongeza sana Mheshimiwa Yahya kwa namna anavyofuatilia suala hili la wanyama wakali na waharibifu na namna anavyowahami na kutoa elimu na yeye kwa wananchi wake.

Mheshimiwa Spika, ninaomba nimtoe shaka Mheshimiwa Yahya kwamba kituo hiki kitajengwa kwa kiwango kikubwa mwaka ujao wa fedha. Sasa hivi Askari wetu wapo site kufanya doria za mara kwa mara ili kuwarejesha hifadhini wanyamapori hao wakali na waharibifu.

Name

Nape Moses Nnauye

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mtama

Primary Question

MHE. YOHANA S. MSITA aliuliza: - Je, upi mpango wa Serikali wa kuondoa kero ya wanyama waharibifu kama tembo kwenye Jimbo la Itigi?

Supplementary Question 4

MHE. NAPE M. NNAUYE: Mheshimiwa Spika, pamoja na maelezo ya Serikali namna wanavyoshughulikia suala la wanyama waharibifu, hasa tembo, nichukue nafasi hii kuipongeza Serikali, kwani zile ndege nyuki kwa Mikoa ya Lindi na Mtwara na hasa Jimbo langu la Mtama, kwa kweli zimekuwa na msaada mkubwa. Tatizo lililopo ni kwamba ndege nyuki zipo kidogo, tatizo likitokea mpaka ije ifukuze wale wanyama inachukua muda mrefu. Je, Serikali iko tayari kuongeza idadi ya ndege nyuki kwenye maeneo yetu?

Name

Hamad Hassan Chande

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kojani

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, Serikali iko tayari, na hivi ninavyozungumza mwaka wa fedha ujao tutaongeza ndege nyuki zisizopungua 100 na tutapeleka katika eneo hilo ndege nyuki kama inavyostahiki.

Name

Boniphace Mwita Getere

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bunda

Primary Question

MHE. YOHANA S. MSITA aliuliza: - Je, upi mpango wa Serikali wa kuondoa kero ya wanyama waharibifu kama tembo kwenye Jimbo la Itigi?

Supplementary Question 5

MHE. BONIPHACE M. GETERE: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru. Kwa umri wa kuishi tembo ni miaka 60 hadi miaka 70 na kuendelea. Kwa kuwa hatuna uwezo wa kuvuna tembo kwa kuwaua, je, lini Serikali itaanzisha uzazi wa mpango kwa kuzuia tembo kuongezeka?

Name

Hamad Hassan Chande

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kojani

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, ni vigumu kuzuia wanyama ambao wanazaa, ni vigumu. Kwa hiyo, kuongozeka kwake kwa sababu ya kizazi, ninaomba tuvumilie tu. Serikali itachukua hatua ya kudhibiti, kujenga uzio ili wasiweze kufika kwenye makazi ya watu.