Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Jacquline Andrew Kainja

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. JACQUELINE K. ANDREW aliuliza:- Je, lini Serikali itatoa elimu ya kutosha kwa wananchi wanaoishi maeneo ya karibu na Hifadhi ya Ugalla Wilaya ya Urambo?

Supplementary Question 1

MHE. JACQUELINE K. ANDREW: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa nafasi niweze kuuliza maswali yangu mawili ya nyongeza. Pamoja na majibu mazuri ambayo Wizara imetupatia, Wilaya yetu ya Urambo katika Hifadhi ya Mto Ugalla imezungukwa na Kata Nne kubwa ambazo zinazunguka hifadhi hiyo, lakini majibu haya hayajaonesha ni namna gani Kata hizi za Kasisi, Ukondamoyo, Nsenda na Ugalla yenyewe itafikiwa na elimu hiyo. Ninataka kujua, ni lini sasa Kata hizi zote zitapatiwa elimu ya uhifadhi?

Mheshimiwa Spika, swali langu la pili. Bado wananchi hawana elimu ya kutosha ya kujihami na wanyama wakali. Je, ni lini Simba na Tembo wataweza kudhibitiwa kutokwenda kwenye makazi ya watu? Ahsante. (Makofi)

Name

Hamad Hassan Chande

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kojani

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, kabla ya kujibu, ninaomba ni mpongeze sana Mheshimiwa Jacqueline kwa namna anavyofuatilia suala hili na anavyo wapambania wananchi wake wa Urambo na Tabora kwa jumla.

Mheshimiwa Spika, suala la kutoa elimu ni suala endelevu na la kila siku. Nimtoe shaka Mheshimiwa Mbunge kwamba zile kata ambazo hazijafikiwa, zitafikiwa ndani ya mwaka huu wa fedha. Kila ambaye hajapata elimu, atapata elimu hiyo kwa njia mbalimbali ambazo tumeziandaa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa swali lake la pili, Serikali kupitia hifadhi zetu zinafanya doria za mara kwa mara katika sehemu zote ili kutoa elimu ya kujihami na wanyama wakali na waharibifu.

Mheshimiwa Spika, nitoe maelekezo kwa Kamishna wetu wa Hifadhi wa TAWA na TANAPA waende Urambo, ambako anasema ndugu yangu Mheshimiwa Mbunge kwamba wanyama hao wako kwenye vijiji sasa hivi, waende kuwaondoa.

Name

Lucy Edward Mwakyembe

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. JACQUELINE K. ANDREW aliuliza:- Je, lini Serikali itatoa elimu ya kutosha kwa wananchi wanaoishi maeneo ya karibu na Hifadhi ya Ugalla Wilaya ya Urambo?

Supplementary Question 2

MHE. LUCY E. MWAKYEMBE: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi kuuliza swali la nyongeza. Kwa kuwa Tanzania imepata bahati mwaka 2027 kuendesha michezo ya AFCON katika upande wa Bara na Zanzibar, ninataka kujua, kwenye upande wa utalii, wafanyabiashara ndogo ndogo na wajasiriamali nao ni sehemu ya fursa ambayo wameipata kwa ugeni utakaoingia. Je, ni elimu gani imetolewa mpaka sasa, au Serikali imejipanga vipi kutoa elimu kwa wafanyabiashara ndogo ndogo pamoja na wajasiriamali, hususan wanawake?

Name

Hamad Hassan Chande

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kojani

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii, imejipanga vya kutosha kupokea mashindano hayo ya AFCON. Hivi ninavyokwambia, wataalamu wetu wako site, wameshaanza mafunzo na taratibu mbalimbali za wajasiriamali wetu ili kusudi waweze kupokea vizuri, na wanapokuja watu kutoka nje kwa ajili ya michezo, wasiwe wameondoka tu na michezo, bali waende kwenye vivutio vyetu na wajasiriamali wetu nao wawe wanufaika kupitia mashindano hayo ya AFCON.

Name

Benjamin Lukubha Ngayiwa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kahama Mjini

Primary Question

MHE. JACQUELINE K. ANDREW aliuliza:- Je, lini Serikali itatoa elimu ya kutosha kwa wananchi wanaoishi maeneo ya karibu na Hifadhi ya Ugalla Wilaya ya Urambo?

Supplementary Question 3

MHE. BENJAMIN L. NGAYIWA: Mheshimiwa Spika, ninashukuru kwa kuniona. Ninaomba kuuliza swali la nyongeza kwa Mheshimiwa Waziri, kwamba kutokana na kukua kwa shughuli za kibinadamu na kuongezeka kwa idadi ya watu katika Mji wa Kahama, je Serikali ina mpango gani wa kumega eneo dogo la Hifadhi ya Pori la Nkweni ambalo lipo kati ya Kahama na Wilaya ya Ushirombo ili kuwapatia wananchi waweze kufanya shughuli zao za kibinadamu kama ufugaji na kilimo?

Name

Hamad Hassan Chande

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kojani

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, eneo ambalo amelitaja kwa sasa, Serikali haina mpango wa kumega kwa ajili ya matumizi ya wanadamu, lakini, kama kuna haja kubwa ambayo anaiona yeye Mheshimiwa Mbunge, basi tukae tu mezani mimi na yeye, twende site tuone. Kama ipo haja ya kufanya hivyo, Serikali inaweza ikachukua hatua siku zijazo.