Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Prof. Joyce Lazaro Ndalichako
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Kasulu Mjini
Primary Question
MHE. PROF. JOYCE L. NDALICHAKO aliuliza: - Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa Barabara ya Kasulu – Kigondo na Habitat – Hwazi, kupitia Mradi wa TACTIC?
Supplementary Question 1
MHE. PROF. JOYCE L. NDALICHAKO: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali ya nyongeza. Swali langu la msingi lilikuwa, ni lini ujenzi wa barabara hizo utaanza? Barabara ya Hwazi – Habitat ni mbaya sana na haitengewi fedha yoyote kwa sababu, tayari ipo kwenye Mpango wa TACTIC. Kwa hiyo, naomba Mheshimiwa Waziri awaambie wananchi wa Kasulu, ni lini mradi huu wa TACTIC, barabara hizo kilometa 5.8 zitaanzwa kujengwa?
Mheshimiwa Spika, swali langu la pili. Tunafahamu mvua kubwa ambazo zinanyesha zimeleta uharibifu mkubwa wa barabara na Jimbo la Kasulu Mjini limeathirika. Kwa mfano, Barabara ya Kasulu – Kabanga – Muganza, Heru Juu – Munyegera na Kanazi – Msambara – Kabanga, zimeharibika na tumeziombea fedha za dharura. Je, ni lini fedha hizo za dharura zitapelekwa ili barabara hizo ziende kutengezwa? Ahsante sana. (Makofi)
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, Halmashauri ya Mji wa Kasulu umewekwa kwenye mpango wa ujenzi wa barabara na miundombinu mingine kupitia TACTIC. Miongoni mwa miji 45, na halmashauri hii iko awamu ya tatu.
Mheshimiwa Spika, tulianza na awamu ya kwanza, utekelezaji unaendelea, awamu ya pili utekelezaji unaendelea na awamu ya tatu tuko hatua za mwisho za usanifu, kwa ajili ya kuanza kupata makandarasi na kuanza ujenzi wa miundombinu hiyo.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Prof. Ndalichako kwamba, Serikali inaendelea kufanya taratibu za ukamilishaji wa usanifu, na mara baada ya kukamilisha usanifu hatua za utekelezaji wa ujenzi wa barabara hizi na miundombinu mingine itaanza mara moja.
Mheshimiwa Spika, swali la pili. Ni kweli kwamba, mvua imeleta athari kwenye barabara zetu na Serikali inaendelea kufanya tathmini mpaka wiki iliyopita. Tunahitaji kiasi cha shilingi bilioni 98, kwa ajili ya ujenzi wa barabara, kwa maana ya dharura, katika maeneo mbalimbali kote nchini ili kurejesha barabara kwenye hali yake ya kawaida.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, barabara hii aliyoitaja ni miongoni mwa barabara ambazo zitapelekewa fedha za dharura ili ziweze kupitika wakati tunasubiri mradi wa TACTIC kuanza kutekelezwa, kama ambavyo imepangwa, ahsante.
Name
Mabula Johnson Magangila
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Msalala
Primary Question
MHE. PROF. JOYCE L. NDALICHAKO aliuliza: - Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa Barabara ya Kasulu – Kigondo na Habitat – Hwazi, kupitia Mradi wa TACTIC?
Supplementary Question 2
MHE. MABULA J. MAGANGILA: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Kwa kuwa, Mji wa Isaka ni bandari kavu ndipo ambapo Station ya SGR inajengwa pale katika Mji wa Kahama, je, ni lini Serikali itaweka mpango wa kuujenga ule mji kwa kiwango cha lami? (Makofi)
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, barabara zetu zinaendelea kujengwa kwa awamu, na Serikali imetambua maeneo yote ambayo yanahitaji kujengwa barabara za changarawe, barabara za lami na tunaendelea kutambua maeneo hayo kulingana na uhitaji, na Serikali inatambua kwamba, Mji wa Isaka ni wa kibiashara unaokua haraka.
Mheshimiwa Spika, ni kweli kuna station ya SGR, lakini pia, shughuli za kiuchumi zimeendelea kuongezeka. Ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, Serikali itaendelea kutenga fedha kwa awamu na kufanya tathmini ili kuweza kujenga barabara hizo kwa kiwango cha lami au changarawe kwa kadri ambavyo itakuwa inawezekana.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved