Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 3 Sitting 13 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Waziri Mkuu-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) 144 2026-04-21

Name

Prof. Joyce Lazaro Ndalichako

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Kasulu Mjini

Primary Question

MHE. PROF. JOYCE L. NDALICHAKO aliuliza: -

Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa Barabara ya Kasulu – Kigondo na Habitat – Hwazi, kupitia Mradi wa TACTIC?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Profesa Joyce Lazaro Ndalichako, Mbunge wa Jimbo la Kasulu Mjini, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Halmashauri ya Mji wa Kasulu ni miongoni mwa halmashauri za miji 45 inayotekeleza Mradi wa TACTIC nchini. Mji wa Kasulu uko kundi la tatu la utekelezaji wa Mradi wa TACTIC lenye miji 18. Katika mradi huu, Halmashauri ya Mji wa Kasulu imetengewa shilingi billioni 10.87.

Mheshimiwa Spika, Mradi wa TACTIC umekamilisha usanifu wa miradi ya Mji wa Kasulu wa Barabara za Makaburi – Kigondo, kilometa 3.77, Habitat – Hwazi, km 2.04, jumla ya kilometa 5.8. Mradi huu unahusisha pia ujenzi wa Stendi ya Mabasi ya Murus na Soko la Kumsenga, Kasulu. Baada ya kukamilisha usanifu wa miradi hii yote, Serikali kwa kushirikiana na Benki ya Dunia inaendelea na taratibu za maandalizi ya kuanza utekelezaji wa miradi katika kundi hili, ikiwemo Halmashauri ya Mji wa Kasulu. Ahsante.