Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Fatma Hassan Toufiq
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. FATMA H. TOUFIQ aliuliza: - Je, Serikali inatoa tamko gani kuhusu wasichana waliopata mimba kutokana na kubakwa na wanaopewa mimba na baba zao na ndugu wa karibu?
Supplementary Question 1
MHE. FATMA H. TOUFIQ: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa majibu mazuri ya Serikali. Pamoja na majibu mazuri nina maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Spika, swali la kwanza, baadhi ya wahanga wa ukatili huu wamekuwa wakijaribu kutoa mimba hizi baada ya kupewa mimba na maharimu wao na hivyo kugharimu maisha yao; je, Serikali inatoa kauli gani kuhusiana na jambo hili?
Mheshimiwa Spika, je, Serikali inawasaidiaje wale wahanga wa ukatili ambao wamepewa mimba na maharimu wao na familia zao zimekuwa zikiwatenga? Ahsante.
Name
Mwanaidi Ali Khamis
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WANAWAKE WA MAKUNDI MAALUM: Mheshimiwa Spika, ahsante, kwanza Serikali inatoa kauli kali kwa wale wote ambao wanapata mimba na kuzitoa. Kwanza utoaji wa mimba ni kosa la jinai Serikali itaendelea kutoa elimu kupitia maafisa wetu wa ustawi wa jamii kuwaelimisha wahanga wote waliopatwa na changamoto za kupata mimba ili waweze kuondokona na msongo wa mawazo na kupata huduma stahiki.
Mheshimiwa Spika, swali lake la pili, Serikali inaendelea kutoa huduma za nyumba salama kwa wahanga ambao wametelekezwa na familia zao, lakini inatoa huduma za afya ya mkono kwa mkono, lakini pia tunatoa huduma za msaada kisheria kwa wahanga hao ili kuhakikisha kwamba wanakaa salama na wanaondokana na misongo ya mawazo na kuendelea na maisha yao, ahsante.
Name
Maryam Azani Mwinyi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. FATMA H. TOUFIQ aliuliza: - Je, Serikali inatoa tamko gani kuhusu wasichana waliopata mimba kutokana na kubakwa na wanaopewa mimba na baba zao na ndugu wa karibu?
Supplementary Question 2
MHE. MARYAM AZAN MWINYI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana, watoto wengi wanaopata mimba za utotoni ni wale watoto ombaomba wa mitaani, je, Serikali ina mkakati gani wa kuwalinda watoto hawa?
Name
Mwanaidi Ali Khamis
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WANAWAKE WA MAKUNDI MAALUM: Mheshimiwa Spika, Serikali ina mpango na ina mkakati wa kuwalinda watoto hawa kwa kuwafuata na kuwahoji baadaye baada ya kuwahoji kwa kuwakutanisha na wazazi wao ili waendelee na maisha na wazazi pale wanaposhindwa basi Serikali ina vituo vyetu vya kulelea watoto ambapo vipo Dodoma, lakini vipo Dar es Salaam na watoto hao wanalelewa na kupata stahiki zote kuanza elimu mpaka wanapokuwa na kutimiza miaka 18 na kuendelea na maisha yao, ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved