Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2020-2025 | Session 19 | Sitting 28 | Other Sectors | Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum | 355 | 2025-05-20 |
Name
Fatma Hassan Toufiq
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. FATMA H. TOUFIQ aliuliza: -
Je, Serikali inatoa tamko gani kuhusu wasichana waliopata mimba kutokana na kubakwa na wanaopewa mimba na baba zao na ndugu wa karibu?
Name
Mwanaidi Ali Khamis
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO, JINSIA, WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM alijibu: -
Mheshimiwa Spika, ubakaji ni kosa la jinai kwa mujibu wa Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, Sheria ya Mtoto, Sura Na.13 pamoja na sheria nyingine zinazopinga ukatili kwa watoto. Serikali kupitia Wizara tunayoisimamia inakemea vikali tabia ya ubakaji na ulawiti wa watoto pamoja na matamko na hatua za kisheria ambazo zimekuwa zikichukuliwa, Serikali imeendelea kutekeleza Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto Awamu ya pili wa mwaka 2024/2025 hadi 2028/2029 ambapo umejikita katika kumaliza ukatili ukijumuisha kubakwa na kupewa mimba kwa kuzini na maharimu au ndugu na jamaa wa karibu ikiwemo baba wa kuzaa, ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved