Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Noah Lemburis Saputi Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Arumeru-Magharibi

Primary Question

MHE. NOAH L. SAPUTU aliuliza: - Je, lini Serikali itakarabati Mnada wa Olokii uliopo Kata ya Bwawani – Arumeru Magharibi?

Supplementary Question 1

MHE. NOAH L. S. MOLLEL: Mheshimiwa Spika, nashukuru, kwanza kwa kuwa nimeuliza swali hili leo ni mara ya tatu, mara ya kwanza majibu yalikuwa ni itawekwa kwenye bajeti ya mwaka 2022/2023, mara ya pili ilikuwa itawekwa kwenye bajeti ya mwaka 2023/2024; lakini leo majibu yaliyokuja ni kwamba wanatafuta hati. Mnada huu umemilikiwa tangu mwaka 1968 - 1970; je, nini kauli ya Serikali kuhusu majibu haya ambayo hayaendani ambayo yameelezwa pia hapa?

Mheshimiwa Spika, swali la pili, kwa kuwa Wizara inakusanya fedha tangu mwaka 1968 - 1970 na mpaka sasa na pale kuna changamoto ya choo, hakuna maji na miundombiinu mingine kama uzio wa mifugo; nini kauli ya Serikali kwamba kutumia fedha ambazo wanazikusanya kwenye mnada huo ili waweze kuweka miundombinu hiyo hasa choo na maji kwa wakati huu wa dharura?

SPIKA: Mheshimiwa Saputu umesema haya majibu hayaendani na swali au ni kwamba majibu yanaendana na swali ila umeshajibiwa hivyo mara kadhaa ili nijue kama maswali yako ya nyongeza yajibiwe au hapana.

MHE. NOAH L. S. MOLLEL: Mheshimiwa Spika, nimesema niliuliza swali hili kwa mara ya tatu leo, lakini jibu lililokuwa la kwanza ilikuwa lipo kwenye bajeti ili ukarabatiwe, lakini jibu la leo limekuja tofauti kwamba wanatafuta mpaka wapate kibali ndiyo waweze kufanya ukarabati.

SPIKA: Sawa, mimi nataka kujua hili jibu kwanza maana ili uulize swali la nyongeza lazima majibu yaliyopo hapa uwe unakubaliana nayo. Sasa haya majibu hapa unakubaliana nayo ili nimpe nafasi ya kujibu ya nyongeza, kama hukubaliani nayo maana yake ndiyo tuanze kutafuta sasa wewe ulikuwa unatafuta nini hapa kwenye swali lako.

MHE. NOAH L. S. MOLLEL: Mheshimiwa Spika, yanaendana kwa sababu si wamesema wanatafuta hati.

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO K.n.y. WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana, kwanza nimuondoe shaka Mheshimiwa Noah Saputu, Mbunge wa Arumeru Magharibi kwamba majibu yote ambayo Serikali tumekuwa tukiyatoa tunayatoa kwa usahihi kwa sababu lengo letu ni kuhakikisha kwamba taratibu zote tunafata ili mnada huu uweze kukamilika na nimthibitishie tu kwamba changamoto chache ambazo zipo katika eneo hilo kama ujenzi wa choo, upatikanaji wa maji ni sehemu ya zile changamoto ndogo ambazo tumekuwa tukizitatua, lakini sisi tunataka Wizara ya Mifugo kufanya ule ukarabati mkubwa ambao utahusisha soko zima. Kwa hiyo, ule ukarabati mkubwa ndiyo unahitaji sasa umiliki wa eneo ndiyo kitu ambacho kikubwa tumekizungumzia.

Mheshimiwa Spika, haya matokeo ya ukarabati mdogo mdogo sijui kama choo kimejaa, maji ya mara moja, hayo yamekuwa yakifanyika na nimthibitishie tu Wizara ya Mifugo italifanya hiyo, ahsante.