Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2020-2025 | Session 19 | Sitting 28 | Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives | Wizara ya Mifugo | 534 | 2025-05-20 |
Name
Noah Lemburis Saputi Mollel
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Arumeru-Magharibi
Primary Question
MHE. NOAH L. SAPUTU aliuliza: -
Je, lini Serikali itakarabati Mnada wa Olokii uliopo Kata ya Bwawani – Arumeru Magharibi?
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO K.n.y. MIFUGO NA UVUVI alijibu:-
Mheshimiwa Spika, ahsante, Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi inawajibu wa kuhakikisha kuwa biashara ya mifugo inafanyika katika mazingira yenye miundombinu muhimu ili kurahisisha biashara hiyo. Aidha, Mnada wa Olokii uliopo katika Kata ya Bwawani, Arumeru Magharibi ni mnada wa upili unaosimamiwa moja kwa moja na Wizara ya Mifugo na Uvuvi na mnada huu hufanya kazi kila Ijumaa ya wiki.
Mheshimiwa Spika, kuhusu ukarabati wa mnada huo Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi ipo katika taratibu za umiliki wa eneo la mnada huo na mara tu taratibu hizo zitakapokamilika Serikali itakua tayari kufanya ukarabati wa mnada huo.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved