Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Soud Mohammed Jumah

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Donge

Primary Question

MHE. MOHAMMED JUMAH SOUD aliuliza: - Je, kwa nini NEMC haianzishi utaratibu wa kuishirikisha ZEMA ili kuongeza ufanisi wa uibuaji na usimamizi wa miradi ya mazingira Zanzibar?

Supplementary Question 1

MHE. MOHAMMED JUMAH SOUD: Mheshimiwa Spika, ahsante sana, pamoja na majibu mazuri ya Serikali, nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, swali namba moja; kwa kuwa mwongozo wa ushirikiano kwa taasisi ambazo siyo za Muungano unazielekeza taasisi ambazo siyo za Muungano kuweza kukutana angalau mara moja katika kila robo mwaka. Je, taasisi hizi za ZEMA na NEMC katika mwaka huu wa fedha wa 2024/2025 zimeshakutana mara ngapi na matokeo yake katika vikao hivyo ni matokeo gani?

Mheshimiwa Spika, kwa swali la pili; nilikuwa nataka kujua, kwa kuwa hizi NEMC na ZEMA ni watoto pacha, mmoja anafanya kazi Tanzania Bara na mmoja anafanya kazi zake Visiwani, ni ndugu hawa.

Mheshimiwa Spika, je, ni miradi mingapi ambayo ameshaitayarisha ambayo inakwenda kutekelezwa na kwa kipindi kilichopita miradi mingapi ambayo imeshapatiwa fedha ambayo wanaitekeleza kwa pamoja ZEMA na NEMC? Ahsante sana.

Name

Khamis Hamza Khamis

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Uzini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Spika, ahsante, niridhie tu kwamba niombe baadaye nifafanue niweze kupata takwimu sahihi ili niweze kumpatia Mheshimiwa Mbunge, ahsante.

Name

Abdul Yussuf Maalim

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Amani

Primary Question

MHE. MOHAMMED JUMAH SOUD aliuliza: - Je, kwa nini NEMC haianzishi utaratibu wa kuishirikisha ZEMA ili kuongeza ufanisi wa uibuaji na usimamizi wa miradi ya mazingira Zanzibar?

Supplementary Question 2

MHE. ABDUL YUSSUF MAALIM: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi kuuliza swali la nyongeza.

Kwa kuwa Zanzibar walishakuwa na Mamlaka ya Mazingira na Uhifadhi, je, ni lini NEMC nao watapata mamlaka kama hayo?

Name

Khamis Hamza Khamis

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Uzini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba Zanzibar wanayo Mamlaka ya Mazingira inaitwa ZEMA, lakini kwa upande wa huku Tanzania Bara tunayo NEMC ambayo bado ni Baraza, nimwambie tu Mheshimiwa Mbunge kwamba mchakato wa kuifanya NEMC kuwa NEMA kwa maana ya kwamba kuwa na mamlaka, mchakato huu umeshaanza na nimwambie tu kwamba wakati utakapofika mchakato huu utafika kwenye Bunge lako Tukufu na tutaujadili kwa pamoja ili lengo na madhumuni tuweze kuipa nguvu zaidi NEMC iweze kuwa na mamlaka.

Name

Simai Hassan Sadiki

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nungwi

Primary Question

MHE. MOHAMMED JUMAH SOUD aliuliza: - Je, kwa nini NEMC haianzishi utaratibu wa kuishirikisha ZEMA ili kuongeza ufanisi wa uibuaji na usimamizi wa miradi ya mazingira Zanzibar?

Supplementary Question 3

MHE. SIMAI HASSAN SADIKI: Mheshimiwa Spika, ahsante, je, ni lini NEMA na ZEMA zitakuwa na ushirikiano wa pamoja ili kwenda kuondosha changamoto za maji ya bahari yanayoweza kuvamia maeneo ya makazi maeneo ya Kaskazini Unguja?

Name

Khamis Hamza Khamis

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Uzini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Spika, ni kweli kumekuwa kuna changamoto sasa ya athari ya mabadiliko ya tabianchi maji ya bahari yanatoka kwenye kina na yanaingia kwenye makazi na mengine yanakwenda kuathiri kwenye maeneo ya vipando ambavyo havistahimili maji ya chumvi.

Mheshimiwa Spika, katika bajeti ambayo tuliiwasilisha hapa tuliisoma na Wabunge hawa wakaipitisha tarehe 25 Aprili, mwaka huu ya 2025/2026 moja ya miongoni mwa mambo ambayo tumesema tutayapa kipaumbele ni kuhakikisha kwamba tunakwenda kutatua changamoto ya maji ya bahari yanayoingia kwenye makazi ikiwemo maeneo ya Nungwi, maeneo ya Sepwese, maeneo ya Mgando, maeneo ya Mtwara na maeneo yote ambayo yanatoka maji ya bahari na yanaingia kwenye makazi.

Mheshimiwa Spika, nimuombe Mheshimiwa awe na subira kazi hii inakwenda kuanza hivi karibuni.