Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2020-2025 | Session 19 | Sitting 28 | Enviroment | Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano | 353 | 2025-05-20 |
Name
Soud Mohammed Jumah
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Donge
Primary Question
MHE. MOHAMMED JUMAH SOUD aliuliza: -
Je, kwa nini NEMC haianzishi utaratibu wa kuishirikisha ZEMA ili kuongeza ufanisi wa uibuaji na usimamizi wa miradi ya mazingira Zanzibar?
Name
Khamis Hamza Khamis
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Uzini
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA alijibu:-
Mheshimiwa Spika, ili kuongeza ufanisi katika uhifadhi na usimamizi wa mazingira katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kumekuwa na utaratibu wa kushirikiana kati ya NEMC na ZEMA katika uibuaji na usimamizi wa miradi ya mazingira. Miradi hiyo ipo katika hatua mbalimbali zikiwemo hatua za maandalizi na utekelezaji.
Mheshimiwa Spika, kwa sasa mradi unaotekelezwa ni mradi wa kuimarisha uwezo wa jamii za pwani kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi. Mradi huu unatekelezwa Unguja na Pemba kwa thamani ya dola za Kimarekani milioni moja. Aidha, miradi miwili inayoandaliwa kwa ushirikiano wa NEMC na ZEMA ni kama ifuatavyo: -
(a) Mradi wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi katika maeneo yenye upungufu wa maji baridi; mradi huu upo katika hatua za kupata kibali cha fedha kutoka Mfuko wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi - Adaptation Fund na utatekelezwa Unguja na Pemba kwa thamani ya dola za Kimarekani milioni 3.5.
(b) Mradi wa kuimarisha miundombinu katika ukanda wa pwani ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi; mradi huu upo katika hatua za kupitishwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika na utatekelezwa Tanzania Bara na Zanzibar, nakushukuru.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved