Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Zuena Athumani Bushiri
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ZUENA A. BUSHIRI aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga Barabara ya Uchira - Kisomachi kwa kiwango cha lami katika Jimbo la Vunjo?
Supplementary Question 1
MHE. ZUENA A. BUSHIRI: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi niulize swali la nyongeza.
Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri ya Serikali, barabara hii ina kilometa 10.9. Barabara hii ni korofi sana kipindi cha mvua, mnamo mwaka 2019 wananchi walijenga kilometa 1.4 kwa nguvu zao na Serikali ikaahidi kwamba itamalizia kilometa zilizobakia. Wananchi wa Vunjo wanataka kujua, je, ni lini Serikali itakamilisha hizo kilometa zilizobakia? Ahsante.
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Spika, dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita ni kuhakikisha inaendelea kuimarisha mtandao wa barabara zetu hizi za wilaya zinazosimamiwa na TARURA na ndiyo maana utaona katika kipindi cha Awamu ya Sita bajeti ya TARURA imeongezeka maradufu. Bajeti ya TARURA ilikuwa ni shilingi bilioni 275 kwa mwaka, lakini tunavyozungumza wakati huu tunatarajia katika mwaka wa bajeti unaokuja 2025/2026 bajeti ya TARURA itakuwa ni shilingi trilioni 1.18.
Mheshimiwa Spika, katika wilaya hii, katika Jimbo hili la Vunjo katika kipindi cha miaka minne tayari zaidi ya shilingi bilioni 10 zimetumika kwa ajili ya kuendeleza miundombinu ya barabara hizi za wilaya, lakini katika mwaka wa fedha unaokuja tayari tunatarajia tutakuwa tuna shilingi bilioni 4.6 kwa ajili ya kuendelea kuimarisha mtandao wa barabara hizi za TARURA.
Mheshimiwa Spika, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Zuena Bushiri kwamba kama vile Serikali ambavyo imekuwa ikitenga fedha kila mwaka wa bajeti kuanzia mwaka 2019/2020, Serikali itaendelea kutenga fedha kwa ajili ya kuhakikisha inakamilisha barabara hii ya Uchira – Kisomachi kwa kiwango cha lami katika Jimbo la Vunjo.
Name
Dr. Charles Stephen Kimei
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Vunjo
Primary Question
MHE. ZUENA A. BUSHIRI aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga Barabara ya Uchira - Kisomachi kwa kiwango cha lami katika Jimbo la Vunjo?
Supplementary Question 2
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana, kwa moyo wa dhati ninaomba nitoe shukrani nyingi kwa Mheshimiwa Mchengerwa, Waziri wa TAMISEMI kwa kutembelea Jimbo la Vunjo, hususani Barabara ya Chekereni – Kahe – Mabogini na kutoa maagizo chanya kuhusiana na ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami.
Mheshimiwa Spika, ninaomba nimuulize Mheshimiwa Naibu Waziri, je, kazi hiyo itaanza lini? (Makofi)
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Spika, kwa hakika Mheshimiwa Dkt. Kimei amekuwa akifanya ufuatiliaji wa karibu sana kuhakikisha kwamba miundombinu ya barabara hizi za wilaya katika jimbo lake inaendelea kuimarishwa. Ninakumbuka mwaka 2024 alileta timu hapa ya watu kutoka jimboni kwake, tukakaa pamoja ofisini kujadili na kutengeneza mipango.
Mheshimiwa Spika, kama alivyosema yeye mwenyewe hivi karibuni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Mheshimiwa Mohamed Mchengerwa, alifika katika Jimbo la Vunjo kwenye ziara na akaagiza kwamba Barabara hii ya Chekereni – Kahe – Mabogini iweze kujengwa kwa kiwango cha lami.
Mheshimiwa Spika, ninaomba nimuhakikishie Mheshimiwa Dkt. Kimei, kwamba, tayari sisi kama Ofisi ya Rais, TAMISEMI tukitumia uratibu wa Mameneja wetu wa TARURA katika ngazi ya mkoa na wilaya tumeanza taratibu kwa ajili ya kuanza kutekeleza maagizo haya ya Mheshimiwa Waziri. Nikuhakikishie Mheshimiwa Mbunge, barabara hii itajengwa ili wananchi wako waweze kupata barabara nzuri ya kufanya shughuli zao za kiuchumi na kufikia huduma muhimu za kijamii.
Name
Dr. Thea Medard Ntara
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ZUENA A. BUSHIRI aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga Barabara ya Uchira - Kisomachi kwa kiwango cha lami katika Jimbo la Vunjo?
Supplementary Question 3
MHE. DKT. THEA M. NTARA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru, eneo la Mpamaa - Msalato, walikuwa wanachonga zile barabara za mitaa. Ni lini sasa mtamalizia kujenga barabara za mitaa katika eneo lile la Mpamaa - Msalato ili wananchi wafike kwenye makazi yao? Ahsante.
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Spika, dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita ni kuendelea kuhakikisha kwamba inaongeza mtandao wa barabara hizi za wilaya ambazo zina umuhimu mkubwa sana kiuchumi, lakini zinaweza kuwasaidia wananchi kufikia huduma za msingi kabisa za kijamii.
Mheshimiwa Spika, ni kweli kabisa Serikali imeanza kuchonga barabara katika eneo la Mpamaa – Msalato na ninaomba nitumie nafasi hii kuendelea kumsisitiza Meneja wa TARURA wa Mkoa na wa Wilaya, wasimamie kwa ukamilifu zoezi hili ili liweze kukamilika nab bb hizi ziweze kufunguka ili wananchi waweze kuzitumia kwa manufaa mapana.
Name
Hawa Mchafu Chakoma
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ZUENA A. BUSHIRI aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga Barabara ya Uchira - Kisomachi kwa kiwango cha lami katika Jimbo la Vunjo?
Supplementary Question 4
MHE. HAWA M. CHAKOMA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru, Barabara ya Jaribu – Mpakani, Kivinje – Nanjache yenye urefu wa kilometa 32 ujenzi wake umesimama, mkandarasi hayupo site na muda wa ujenzi ulishakwisha. Ni nini kauli ya Serikali juu ya kadhia hii?
Name
Zainabu Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Spika, ninaomba nitumie nafasi hii kumkumbusha Meneja wa TARURA Mkoa wa Pwani pamoja na Meneja wa TARURA ngazi ya Wilaya waweze kufanya ufuatiliaji wa karibu kabisa ili waweze kujua changamoto ni nini ambayo inafanya mkandarasi asiwepo site, lakini waweze kuamua changamoto iliyojitokeza. Wawasiliane na sisi kama kuna changamoto ambayo iko juu ya uwezo wao ili tuweze kuikwamua barabara hii iweze kujengwa na mkandarasi arudi site. (Makofi)
Name
Aida Joseph Khenani
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Nkasi Kaskazini
Primary Question
MHE. ZUENA A. BUSHIRI aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga Barabara ya Uchira - Kisomachi kwa kiwango cha lami katika Jimbo la Vunjo?
Supplementary Question 5
MHE. AIDA J. KEHANI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru, Barabara ya Namanyere – Mashete imekuwa na changamoto kwa muda mrefu. Ni upi mkakati wa Serikali wa kuikarabati kwa sasa?
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Spika, Serikali ya Awamu ya Sita imekuwa ikitenga bajeti kwa kila mwaka wa fedha kwa ajili ya kuhakikisha inaendelea kuimarisha barabara hizi za wilaya zinazosimamiwa na TARURA. Ni dhahiri kabisa utaona kuna ongezeko la bajeti. Tangu Serikali ya Awamu ya Sita ilipoingia madarakani ilikuta bajeti ya TARURA kwa mwaka ni shilingi bilioni 275, lakini hivi tunavyozungumza tunatarajia bajeti ya TARURA katika mwaka wa fedha 2025/2026 itakuwa ni shilingi trilioni 1.18.
Mheshimiwa Spika, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Aida Khenani, kwamba barabara hii katika eneo hili la Namanyere itajengwa ili iweze kuwanufaisha wananchi wako na waweze kufanya shughuli zao za kiuchumi, lakini waweze kufikia huduma za kimsingi za kijamii.
Name
Grace Victor Tendega
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ZUENA A. BUSHIRI aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga Barabara ya Uchira - Kisomachi kwa kiwango cha lami katika Jimbo la Vunjo?
Supplementary Question 6
MHE. GRACE V. TENDEGA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana, kwanza ninaipongeza Serikali ya Chama Cha Mapinduzi kwa kutujengea kilometa 33 ya barabara kutoka Iringa Mjini kupitia Kalenga kwenda Kilolo. (Makofi)
Sasa barabara ya kutoka Mtandika kwenda Nyanzwa ambayo ni kilometa 40; ni lini mtaijenga hata kwa kiwango cha changarawe? (Makofi)
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Spika, ni dhahiri Mheshimiwa Grace Tendega anaona kazi kubwa inayofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita katika kuimarisha barabara zetu hizi (mtandao wa barabara za TARURA) ambazo ni muhimu sana kiuchumi na zinawawezesha wananchi kufikia huduma za kimsingi za kijamii.
Mheshimiwa Spika, kama vile ambavyo umeshuhudia Serikali imekuwa ikifanya kazi kubwa ya kuimarisha mtandao wa barabara hizi za TARURA, naomba nikuhakikishie kwamba Barabara hii ya Mtandika kwenda Nyanzwa itaweza kujengwa katika hadhi nzuri. Serikali itafika ili kuhakikisha kwamba wananchi wanapata miundombinu mizuri ya barabara.