Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2020-2025 | Session 19 | Sitting 28 | Regional Administration and Local Government Authorities | Ofisi ya Rais TAMISEMI. | 352 | 2025-05-20 |
Name
Zuena Athumani Bushiri
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ZUENA A. BUSHIRI aliuliza:-
Je, lini Serikali itajenga Barabara ya Uchira - Kisomachi kwa kiwango cha lami katika Jimbo la Vunjo?
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, Serikali ilianza kutekeleza ujenzi wa Barabara ya Uchira – Kisomachi - Kolarie kwa kiwango cha lami mwaka 2019/2020 ambapo kilometa 1.4 zilijengwa kwa shilingi milioni 694.575. Aidha, mwaka 2023/2024 shilingi milioni 724 zilitolewa kwa ajili ya kujenga kipande chenye urefu wa kilometa 0.8 ambapo kazi imefikia 40%. Katika mwaka 2024/2025 Serikali imeendelea na ujenzi wa tabaka la lami kwa urefu wa kilometa 0.8 kwa gharama ya shilingi milioni 474.56. Ujenzi unaoendelea sasa utakapokamilika utafanya jumla ya urefu wa kilometa 3.0 za lami kuwa zimekamilika.
Mheshimiwa Spika, vilevile katika mwaka 2025/2026 Serikali imepanga kujenga kilometa moja kwa kiwango cha lami kwa shilingi milioni 500. Serikali itaendelea kuihudumia miundombinu ya barabara na madaraja katika Jimbo la Vunjo kwa kujenga, kukarabati na matengenezo kulingana na upatikanaji wa fedha.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved