Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Dr. Pius Stephen Chaya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Manyoni
Primary Question
MHE. DKT. PIUS S. CHAYA aliuliza:- Je, kuna mpango gani wa kurasimisha viongozi wa nyumba kumi (mabalozi) kama sehemu ya kuimarisha usalama wa raia?
Supplementary Question 1
MHE. DKT. PIUS S. CHAYA: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri ya Serikali ninayo maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Spika, swali la kwanza; kwa kuwa Serikali imekiri kwamba mabalozi nao ni sehemu muhimu ya kuimarisha ulinzi na usalama na maendeleo ya halmashauri zetu, sasa nini mpango wa Serikali kuhakikisha kwamba wanatumia kada hii ya mabalozi kuwajengea uwezo?
Mheshimiwa Spika, swali la pili; kwa kuwa mwaka jana ulikuwa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na tayari tulishapata Wenyeviti wa Vijiji, Mitaa na Vitongoji nini mkakati wa Serikali kuhakikisha kwamba wanawajengea uwezo? Ahsante sana.
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, ahsante sana, ni kweli kwamba, Viongozi wa Serikali za Mitaa wakiwemo Mabalozi, Waheshimiwa Wenyeviti wa Vijiji, Vitongoji na Mitaa ni nguzo muhimu katika usalama wa raia katika maeneo yao. Hata hivyo, jambo la msingi kwanza usalama unaanza kwa kila mwananchi mwenyewe kutimiza wajibu wake na kutoa taarifa pale anapoona kuna viashiria vya kuathirika kwa usalama katika eneo hilo na mabalozi ndiyo viongozi wa kwanza katika mitaa yetu ambao wanapokea taarifa hizo ambazo zinafanyiwa kazi kwa ngazi ya ubalozi, kijiji, mtaa na hatua zinazofuata ngazi ya kata mpaka wilaya, mpaka ngazi ya Taifa.
Mheshimiwa Spika, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali imeendelea kuwajengea uwezo Waheshimiwa Mabalozi na wanafanya kazi zao, lakini zoezi hili ni endelevu. Tutaendelea kuwajengea uwezo mara kwa mara ili wawe na ufanisi mkubwa zaidi katika kutambua viashiria vinavyoathiri usalama, lakini pia kuchukua hatua stahiki kwa wakati ili kuhakikisha kwamba jamii yetu inakuwa salama zaidi. Hivyo hivyo, viongozi ambao wamechaguliwa mwaka 2024, Wenyeviti wa Vijiji, Mitaa na Vitongoji wataendelea kujengewa uwezo huu ili kuwa na uwezo mzuri zaidi wa kusimamia masuala ya usalama, ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved