Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Mvita Mustafa Ali

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

Je, Serikali ina mpango gani wa kuwaendeleza... MWENYEKITI: Mheshimiwa Mbunge unataja tu namba ya swali na unaomba swali lako lijibiwe. MHE. MVITA MUSTAFA ALI aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kuwaendeleza walengwa wa TASAF waliopata ruzuku ya uzalishaji na kutolewa baada ya kuhitimu mpango huo?

Supplementary Question 1

MHE. MVITA MUSTAFA ALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana na nina maswali mawili ya nyongeza.

Swali langu la kwanza linasema; kuna wanufaika wangapi wanawake ambao wamehitimu katika mpango huo?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili linasema; je, unaweza kuliambia Bunge hali zao hao wanufaika kiuchumi katika mpango huu kwa ujumla wake?

Name

Regina Ndege Qwaray

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza ninampongeza Mheshimiwa Mbunge kwa maswali yake mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mpango wa kunusuru kaya maskini ni kuhakikisha kwamba walengwa wanapatiwa uwezo na mwisho wa siku wana uwezo wa kujitegemea. Kwa kufikia hivyo, Serikali imefanya tathmini ya kutosha na kubaini kaya 431,730 ambao tayari wameweza kujitegemea na sasa hawategemei tena ruzuku ya Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kaya hizo wapo wanawake 757,730 ambao wameweza sasa kusimama na kujitegemea kiuchumi. Hata hivyo, swali lake la pili linasema hali za kiuchumi, hali zao za kiuchumi kwa hawa walengwa ni nzuri na wanaendelea kuimarika kwa kufuatiliwa kwa karibu na mamlaka za halmashauri za vijiji na mamlaka za halmashauri zetu za mitaa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ninataka kumhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba walengwa waliohitimu baada ya kuwezeshwa wapo, lakini pale walipowezeshwa basi wameendelea kusimama vizuri.

Mheshimiwa Mweyekiti, ninaendelea kutoa wito na kukumbusha halmashauri zetu nchini kwamba waendelee kufuatilia kaya hizi kwa karibu ili kuhakikisha kwamba zile kaya zinaendelea kuimarika lakini waweze kuwaunganisha na fursa zinazopatikana ndani ya halmashauri ikiwemo mikopo ya 10%; 4/4/2 ili waweze kuendelea kujitegemea kiuchumi badala ya kutegemea ruzuku ya Serikali, ahsante.

Name

Neema Gerald Mwandabila

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

Je, Serikali ina mpango gani wa kuwaendeleza... MWENYEKITI: Mheshimiwa Mbunge unataja tu namba ya swali na unaomba swali lako lijibiwe. MHE. MVITA MUSTAFA ALI aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kuwaendeleza walengwa wa TASAF waliopata ruzuku ya uzalishaji na kutolewa baada ya kuhitimu mpango huo?

Supplementary Question 2

MHE. NEEMA G. MWANDABILA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, nilitaka kufahamu ni sheria ipi inatumika kuwabana wale wote ambao wanaingiza walengwa fake kwenye hii programu ya TASAF na wale wananchi wenyewe ambao wanajijua wana uwezo halafu wanaingia kwenye hiyo programu wanachukuliwa hatua gani? Ahsante. (Makofi)

Name

Regina Ndege Qwaray

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Neema.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza mfumo wa kupata walengwa ambao wanatakiwa kujiunga na TASAF ni shirikishi. Wananchi wamekuwa wakishirikishwa kupitia Serikali zao za vijiji na mitaa ili kuwabaini walengwa wenye sifa wa kujiunga na mfumo huo au na mpango ule wa kunusuru kaya maskini. Hata hivyo, yapo maeneo ambayo yamebainika kwamba watu wanaingia kwenye mfumo huo ambao hawana sifa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imeendelea kufanya tathmini na kuwabaini na pale inapobainika kwamba mlengwa aliyewekwa kwenye mpango hana sifa basi mara moja anaondolewa kwenye mpango. Pia, Serikali imeendelea kuchukua hatua hasa kwa viongozi wale wa Serikali za Mitaa wakiwepo Watendaji wa Vijiji na Watendaji wa Kata ambao wamehusika katika kuingiza watu kwenye mpango ambao hawana sifa basi wameendelea kuchukuliwa hatua za kinidhamu na mamlaka zao za utumishi na pale inapotambulika au inapofahamika kwamba kuna njia zilizotumika za rushwa basi wameendelea kuchukuliwa hatua na mamlaka husika zinazoshughulikia masuala mazima ya rushwa. (Makofi)

Name

Maryam Azani Mwinyi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

Je, Serikali ina mpango gani wa kuwaendeleza... MWENYEKITI: Mheshimiwa Mbunge unataja tu namba ya swali na unaomba swali lako lijibiwe. MHE. MVITA MUSTAFA ALI aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kuwaendeleza walengwa wa TASAF waliopata ruzuku ya uzalishaji na kutolewa baada ya kuhitimu mpango huo?

Supplementary Question 3

MHE. MARYAM AZAN MWINYI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa swali dogo la nyongeza.

Je, Serikali ina mpango gani wa kuzindua Awamu ya Tatu ya Mpango wa Kaya Maskini hapa nchini? (Makofi)

Name

Regina Ndege Qwaray

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Maryam Mwinyi kuwa Serikali kwa sasa imekamilisha, tuko hatua ya mwisho kabisa ya kwenda kuanza Mpango wa Awamu ya Tatu ya Kunusuru Kaya Maskini na mpango huo uko kwenye hatua za mwisho kuhakikisha kwamba tunakwenda kutekeleza ili utekelezaji uanze kwa haraka. Mpango huu wa awamu ya tatu, ni kwenda kuboresha yale mapungufu yaliyojitokeza kwenye awamu ya pili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali tayari imeshakamilisha, ni utekelezaji unakwenda kuanza hivi karibuni.