Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 3 Sitting 10 Good Governance Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora) 104 2026-04-16

Name

Mvita Mustafa Ali

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

Je, Serikali ina mpango gani wa kuwaendeleza...

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mbunge unataja tu namba ya swali na unaomba swali lako lijibiwe.

MHE. MVITA MUSTAFA ALI aliuliza: -

Je, Serikali ina mpango gani wa kuwaendeleza walengwa wa TASAF waliopata ruzuku ya uzalishaji na kutolewa baada ya kuhitimu mpango huo?

Name

Regina Ndege Qwaray

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mvita Mustafa Ali, Mbunge wa Viti Maalum.

Mheshimiwa Mwenyekiti, utekelezaji na ufuatiliaji wa shughuli za Mpango wa TASAF hufanywa na halmashauri husika chini ya uratibu wa TASAF ambapo wanufaika wa mpango hupatiwa mafunzo na kufuatiliwa kwa karibu baada ya kuhitimu mpango ili kuhakikisha wanafikia malengo waliojiwekea.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali itahakikisha kuwa walengwa wa TASAF waliohitimu mpango baada ya kupata ruzuku ya uzalishaji wanakuwa sehemu ya uchumi endelevu kwa kuwasaidia kujiunga na mifumo ya kifedha, kupata masoko na kuendeleza stadi za ujasiriamali ili kuwabadilisha kutoka walengwa wa ruzuku kuwa wajasiriamali wenye uwezo wa kujitegemea, ahsante.