Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Morris Joseph Makoi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Moshi Mjini

Primary Question

MHE. MORRIS J. MAKOI aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga Barabara ya Mbokomu - Mti Mrefu kilometa 13.94 kwa kiwango cha lami ili kuchochea utalii?

Supplementary Question 1

MHE. MORRIS J. MAKOI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa majibu mazuri na ya kutia moyo ya Serikali. Nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa vile barabara ya Rau Madukani - Mamboleo - Materuni - Shimbwe yenye urefu wa kilometa 16.7 ni barabara ambayo ilikuwa ni ahadi ya Mheshimiwa Rais aliyowaahidi watu wa Uru Mashariki na Shimbwe kwamba itajengwa kwa kiwango cha lami kwa maana ya mwendelezo, lakini hiyo barabara ndiyo ambayo inaenda kwenye maanguko makubwa ya maji katika Wilaya ya Moshi na maanguko haya yanachochea sana pato la utalii kwa Halmashauri ya Moshi na wanaingiza karibu shilingi milioni 25 kwa mwezi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, je, Serikali ina mpango gani pamoja na kukamilisha ahadi ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan, ina mpango gani kuhakikisha basi barabara hii pamoja na kujenga lami kiwango cha meta 500, 500, ina mpango gani kuhakikisha sehemu inayobaki inapitika muda wote ili kusaidia watalii kufika kwenye maanguko hayo, kuwasaidia wananchi kusafirisha mazao yao, lakini kikubwa zaidi kuchochea uchumi wa wananchi na utalii kwa ujumla?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, Wilaya ya Moshi ina vijiji 40 ambavyo vimezunguka Mlima Kilimanjaro. Hivi vijiji 40 ndivyo ambavyo vinabaki na madhila yote ya kuzima moto na mahangaiko yote panapotokea uharibifu ndani ya Mlima Kilimanjaro.

Mheshimiwa Mwenyekiti, je, Serikali ina mpango gani wa kutenga 20% mpaka 30% ya mapato ya KINAPA au utalii wa Mlima Kilimanjaro kusaidia maendeleo ya vijiji 40 vinavyozunguka mlima kama vile ujenzi wa barabara ambazo zimeharibika sana, lakini vilevile ujenzi wa vyoo katika taasisi za umma ambazo Waziri Mkuu, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Nchemba, anapigia upatu kwa kiwango kikubwa kuhakikisha kwamba hakuna ukosefu wa vyoo katika shule za sekondari na msingi, lakini pia kukarabati shule za sekondari na msingi katika maeneo hayo?

Mheshimiwa Mwenyekiti, hilo ndiyo swali langu la pili.

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, kwanza, ninampongeza sana Mheshimiwa Morris Joseph Makoi, Mbunge wa Jimbo la Moshi Vijijini kwa namna ambavyo kwa kweli anafanya kazi kubwa ya kuwasemea Wananchi wa Moshi Vijijini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimhakikishie tu kwamba Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, siku zote akitoa ahadi na maelekezo yanatekelezwa. Sisi Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, tulishachukua agizo la Mheshimiwa Rais la kujenga barabara hiyo ambayo Mheshimiwa Mbunge ameitaja na tunafahamu tutakwenda kuijenga kwa awamu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tayari hivi sasa tumeshaiweka kwenye vipaumbele vya Wizara yetu kupitia TARURA kwa ajili ya kuanza ujenzi kwa awamu ili kuhakikisha kwanza wananchi wanapata huduma bora za usafiri na usafirishaji, lakini pili tunaendeleza na kuboresha huduma za utalii, lakini pia na huduma nyingine kama Mheshimiwa Mbunge alivyosema.
Kwa hiyo, Mheshimiwa Mbunge, ninakuhakikishia barabara hiyo ipo kwenye vipaumbele vya Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pili, ni kweli kwamba Mlima Kilimanjaro unazungukwa na vijiji hivyo takribani 40 na tunafahamu kwamba kuna mashirikiano kati ya wananchi, lakini na taasisi za Serikali na taasisi binafsi. Tunaendelea kuhakikisha kwamba kupitia TANAPA na Wizara ya Maliasili na Utalii, tutaendelea kuongea nao na kuwasiliana nao kuona namna nzuri ya kushirikiana katika kuboresha mazingira ya huduma za jamii, barabara, lakini na mambo mengine kwa vijiji hivi ambavyo vinazunguka Mlima Kilimanjaro.

Name

Japhet Ngailonga Hasunga (CPA)

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Vwawa

Primary Question

MHE. MORRIS J. MAKOI aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga Barabara ya Mbokomu - Mti Mrefu kilometa 13.94 kwa kiwango cha lami ili kuchochea utalii?

Supplementary Question 2

MHE. JAPHET N. HASUNGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, kwanza, tunaishukuru Serikali kwa kujenga barabara ya kutoka Vwawa hadi Ndolezi kwa kiwango cha lami. Ni lini sasa Serikali itaendeleza kujenga kuanzia Ndolezi – Mlangali – Shomola – Iyula? (Makofi)

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Mheshimiwa Hasunga amekuwa mfuatiliaji wa karibu sana wa masuala ya jimbo lake la Vwawa lakini pia barabara. Ninakuhakikishia Mheshimiwa Mbunge, kama ulivyosema tayari Serikali imeshajenga barabara hiyo, lakini tunafahamu bado tunahitaji kuendelea na ujenzi. Ninaomba nikuhakikishie kwamba safari ni hatua, tunaendelea kutenga bajeti kwa awamu na lengo la Serikali ni kuhakikisha barabara hiyo inajengwa kiwango cha lami, ili kuwezesha wananchi wa Vwawa na maeneo mengine jirani kupata huduma bora za usafiri.

Name

Asia Abdulkarim Halamga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MORRIS J. MAKOI aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga Barabara ya Mbokomu - Mti Mrefu kilometa 13.94 kwa kiwango cha lami ili kuchochea utalii?

Supplementary Question 3

MHE. ASIA A. HALAMGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Barabara ya Mogitu - Balang'dalalu - Lalaji yenye urefu wa kilometa 45 ni barabara yenye msingi sana kwa uchumi wa Wilaya ya Hanang. Je, ni lini Serikali itaanza ukarabati wa barabara hii?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, ni kweli kwamba barabara hii ya Mogitu - Balang'dalalu ambayo ipo katika Jimbo la Hanang ambalo lina msemaji mahiri sana Mheshimiwa Asia Halamga, mwakilishi bora kabisa wa wananchi wa jimbo hilo, ameshaleta hoja hiyo mara kadhaa Serikalini. Sisi Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, tumeshaiweka kwenye mpango kwa ajili ya ujenzi. Tunafahamu barabara hii haijajengwa muda mrefu na ni barabara muhimu sana kwa shughuli za uchumi na kijamii. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge na wananchi wa Hanang' kwamba Serikali hii sikivu ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan imeweka kipaumbele kwa ajili ya ujenzi wa barabara hiyo kwa awamu.

Name

Fadhili Sandali Chilombe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduru Kusini

Primary Question

MHE. MORRIS J. MAKOI aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga Barabara ya Mbokomu - Mti Mrefu kilometa 13.94 kwa kiwango cha lami ili kuchochea utalii?

Supplementary Question 4

MHE. ENG. FADHILI S. CHILOMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, alivyofika Tunduru alitoa ahadi ya kujengwa Barabara ya Misechela - Tunduru. Barabara hii ni kati ya barabara ambazo zinatoa uzalishaji mkubwa sana wa korosho. Je, Serikali ina mpango gani wa kutekeleza ahadi hiyo?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Tunduru Kusini amekuwa akifuatilia sana suala la ujenzi wa barabara hiyo na sisi tunafahamu kwamba hiyo ni ahadi ya Mheshimiwa Rais, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan. Sisi ahadi za viongozi wetu wa kitaifa ni kipaumbele nambari moja.

Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba tutaendelea kutenga fedha kuhakikisha barabara hiyo inajengwa na dhamira ya Serikali na Mheshimiwa Rais kuwatumikia na kuwahudumia wananchi wa Tunduru inafikiwa.

Name

Marirta Gido Kivunge

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MORRIS J. MAKOI aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga Barabara ya Mbokomu - Mti Mrefu kilometa 13.94 kwa kiwango cha lami ili kuchochea utalii?

Supplementary Question 5

MHE. MARIRTA G. KIVUNGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru sana, je, ni lini barabara ya lami ya kutoka Elerai – Kamwanga, Wilayani Longido itaanza kujengwa? (Makofi)

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ninampongeza Mheshimiwa Mbunge na ninaomba tu nimhakikishie kwamba barabara zote za kimkakati ambazo zina umuhimu mkubwa wa shughuli za kiuchumi na kijamii katika halmashauri zetu kote nchini, ikiwemo Halmashauri ya Longido zinaendelea kutengewa fedha kwa awamu ili kuhakikisha kwamba zinajengwa aidha kiwango cha changarawe au kiwango cha lami kwa kadri ya upatikanaji wa fedha. Kwa hivyo, nimkuhakikishie kwamba hiyo barabara itaendelea pia kutengewa fedha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini nitumie nafasi hii kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, kumuelekeza meneja wa TARURA Mkoa wa Arusha na Wilaya ya Longido, kuifanyia tathmini barabara hiyo na kuwasilisha mpango kazi ambao wame-internalize ndani ya mkoa na sisi ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI tuweze kuona namna ya kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara hiyo.