Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 3 | Sitting 10 | Regional Administration and Local Government Authorities | Ofisi ya Waziri Mkuu-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) | 103 | 2026-04-16 |
Name
Morris Joseph Makoi
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Moshi Mjini
Primary Question
MHE. MORRIS J. MAKOI aliuliza: -
Je, lini Serikali itajenga Barabara ya Mbokomu - Mti Mrefu kilometa 13.94 kwa kiwango cha lami ili kuchochea utalii?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Morris Joseph Makoi, Mbunge wa Moshi Vijijini, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inatambua umuhimu wa Barabara ya Mbokomu – Mti Mrefu katika Wilaya ya Moshi. Katika mwaka wa fedha 2024/25 Serikali ilitenga bajeti ya shilingi milioni 200 kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami nzito (asphalt concrete) mita 200 na tayari zimekamilika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha 2026/2027, Serikali imetenga bajeti ya shilingi milioni 225 kwa ajili ya ujenzi ya barabara hiyo kwa urefu wa meta 200.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kutokana na mahitaji makubwa ya matengenezo ya barabara kiwango cha lami, Serikali itaendelea kutenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara hii kwa awamu, ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved