Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Suma Ikenda Fyandomo
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. SUMA I. FYANDOMO aliuliza: - Je, lini Serikali itakamilisha Ujenzi wa Barabara ya Uyole - Nsalaga - Ifisi mpaka Uwanja wa Ndege Songwe?
Supplementary Question 1
MHE. SUMA I. FYANDOMO Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Kwanza, ninaishukuru Serikali kwa kutuletea Meneja wa TANROADS, Engineer Suleiman Ishanga, anafanya kazi nzuri sana. Kila akisikia barabara zimekorofisha ndani ya Mkoa wa Mbeya, anahamisha na timu yake ili kuhakikisha barabara zinarekebishwa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la kwanza, barabara hiyo ya njia nne ya kuanzia Uyole mpaka Uwanja wa Ndege wa Songwe ambayo ni ya muhimu sana, ina miaka mitano. Serikali imetoa fedha kiasi cha shilingi bilioni 44 wakati bajeti ya barabara hiyo ni shilingi bilioni 183. Ndani ya miaka mitano ni shilingi bilioni 44.
Mheshimiwa Mwenyekiti, majibu ya Serikali yanadai kwamba katika miezi michache iliyobaki kufika Januari, barabara itakuwa imekamilika. Mkandarasi mpaka ninavyoongea sasa hivi, kwa sababu hajapata fedha, amekusanya mitambo yake, amekaa…
MWENYEKITI: Swali lako.
MHE. SUMA I. FYANDOMO Mheshimiwa Mwenyekiti, je, wananchi wa Mkoa wa Mbeya, wanataka kujua ni lini Serikali itampatia fedha mkandarasi huyo ili aendelee na ujenzi wa barabara nne ya Mkoa wa Mbeya? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la pili, kuna barabara ya muhimu sana inayotoka Mbalizi - Chang'ombe kutokea Mkwakajuni, ni lini Serikali itajenga barabara hiyo kwa kiwango cha lami?
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara ya njia nne ya Mji wa Mbeya ama Jiji la Mbeya, tunajua ni Tan-Zam One. Kwa kutambua umuhimu wake na changamoto zilizopo Mkoa wa Mbeya na hasa Jiji la Mbeya, ndiyo maana Serikali imeamua kuijenga kipande hicho cha njia nne.
Mheshimiwa Mwenyekiti, moja ya changamoto kubwa ambayo imefanya barabara hii ichelewe, ilikuwa ni kuondoa miundombinu ya umeme, mkongo, majisafi, na maji machafu ambayo yalikuwa yanapita pale. Kwa hiyo, imechukua muda na mpaka tunavyoongea sehemu nyingine, bado hatujaondoa, kwa sababu lazima tuondoe ndiyo tuanze kuijenga barabara. Hata hivyo, tumeshafikisha 41.7%.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge na wananchi wa Mkoa wa Mbeya na wote wa nyanda za juu kusini kwamba tunavyoongea sasa hivi yapo maandalizi ya hivi karibuni ambayo mkandarasi atapewa fedha ili aweze kuendelea na kazi ya kukamilisha hiyo barabara.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kipindi hiki nyanda za juu kusini zina mvua nyingi sana ambayo kwa earthwork kwa maana ya kazi ya kutengeneza barabara inakuwa ni ngumu sana. Kuhusu Barabara ya kutoka Mbalizi kwenda Mkwakajuni, iko kwenye mpango, na tumeshatangaza kilometa za kwanza, tutakwenda kwa awamu. Tumeshatangaza katika bajeti tunayoendelea nayo na tutaendelea pia na bajeti hii ya 2026/2027 ikiwa ni kuunganisha Mbalizi - Mkwajuni hadi Makongorosi.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved