Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 3 | Sitting 9 | Works and Transport | Wizara ya Ujenzi | 97 | 2026-04-15 |
Name
Suma Ikenda Fyandomo
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. SUMA I. FYANDOMO aliuliza: -
Je, lini Serikali itakamilisha Ujenzi wa Barabara ya Uyole - Nsalaga - Ifisi mpaka Uwanja wa Ndege Songwe?
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Suma Ikenda Fyandomo, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, ujenzi kwa kiwango cha lami wa Barabara ya Uyole kuanzia pale Nsalaga hadi Ifisi yenye urefu wa kilometa 26 kwa njia nne unaendelea, na umefikia 41.7%. Mradi huu unatarajiwa kukamilika tarehe 23 Januari, 2027. Kwa sehemu iliyobaki ya Ifisi hadi Uwanja wa Ndege wa Songwe ambayo ina urefu wa kilometa 3.7, Serikali inatafuta fedha kwa ajili ya kujenga hicho kipande ambacho kitakuwa kimesalia.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved