Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Subira Khamis Mgalu
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. SUBIRA K. MGALU aliuliza: - Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Barabara ya Tamko - Mapinga kwa kipande kilichosalia?
Supplementary Question 1
MHE. SUBIRA K. MGALU: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali madogo mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru kwa majibu ya Serikali ambayo yameainisha kwamba ile awamu ya kwanza zaidi ya kilometa nane tumeona lami, na wanaendelea kumalizia. Kwa kuwa Serikali imesema kilometa 14.62, na kwa kuwa Serikali iliingia mkataba na Kampuni ya Kings Builders Limited kwa thamani ya shilingi bilioni 17, na kwa kuwa mkandarasi huyu alianza hii kazi ilimlipa takribani 1.6 billion, na kwa kuwa mkandarasi huyu anadai madai ya certificate ya kwanza ya 1.1 billion, na ni ya muda mrefu na ikamfanya aondoke site, je, ni lini Serikali italipa hati hii ili aweze kurejea site na kuweza kutimiza ahadi waliyoweka kwamba Juni, 2027 barabara hii itakamilika, na ukizingatia wakazi wa Jimbo la Bagamoyo kuelekea Makao Makuu ya Mkoa wanapata shida; barabara hii katika sehemu hiyo ambayo bado haijakamilika imeharibika sana kipindi hiki cha mvua? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili. Kwa kuwa Kata hii ya Mapinga pia kuna Daraja la Mpiji Chini, na kwa kuwa Serikali iliingia makubaliano (mkataba) na Kampuni ya China Railways Service Group mwaka 2023 ya ujenzi wa daraja hii kwa thamani ya shilingi bilioni 18, kwa kuwa wakati wa ziara ya aliyekuwa Waziri wa Ujenzi, Mheshimiwa Bashungwa Serikali ilivunja mkataba na Kampuni hii, lakini kwa kuwa bado changamoto ni kubwa...
MWENYEKITI: Ninaomba uulize swali.
MHE. SUBIRA K. MGALU: Je, Serikali inatupa taarifa gani ya ujenzi wa daraja hili kwa sasa ili kuwaondolea taabu wananchi wa Kiharaka, Tungutungu, Kiembeni na Minazi Minane, daraja linalounganisha Bagamoyo na Kinondoni Mkoa wa Dar es Salaam? (Makofi)
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakubaliana na Mheshimiwa Mbunge kwamba ujenzi wa barabara umechukua muda. Pia, kama nilivyojibu katika swali langu la msingi kwamba Serikali, labda nitasoma tena, Serikali imeahidi kuipa kipaumbele barabara hii ikiwa ni sehemu mojawapo ya kupunguza msongamano.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba ni kweli barabara nyingi zilikuwa zinasuasua. Kipaumbele chetu sasa hivi ni kuhakikisha kwamba miradi yote inakamilika, ikiwa ni pamoja na daraja ambalo tulikuwa tumetangaza, lakini mkandarasi alishindwa kukamilisha taratibu za kimkataba ikalazimika asimame. Kwa hiyo, daraja linakwenda kujengwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia barabara hii tunahakikisha kwamba tunakwenda kuikamilisha kama tulivyoahidi, kwa sababu hata sisi kama Serikali tunaona ni muhimu sana barabara hii ijengwe, na iweze kupitika katika kipindi hiki, kwa kuwa tunajua itakuwa ni moja ya sehemu ya kupunguza msongamano katika barabara yetu ya Dar es Salaam - Morogoro ikiwa ni pamoja na kulijenga hilo daraja tena baada ya kuachana na mkandarasi. (Makofi)
Name
Festo Richard Sanga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Makete
Primary Question
MHE. SUBIRA K. MGALU aliuliza: - Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Barabara ya Tamko - Mapinga kwa kipande kilichosalia?
Supplementary Question 2
MHE. FESTO R. SANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Naibu Waziri atakubaliana na mimi kwamba ni miaka mitatu Barabara ya Makete - Mbeya haijapata lami hata theluthi moja. Vilevile, Serikali ilikuwa inadaiwa na mkandarasi, na niipongeze kwamba imemlipa mkandarasi, lakini hadi sasa hakuna dalili zozote kwamba mkandarasi anaweza akaendelea kujenga barabara hiyo licha ya kwamba amelipwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni yapi maelekezo ya Waziri na Serikali kwa ujumla kwa mkandarasi huyu kwa ajili ya barabara ya Wananchi wa Makete kutoka Mbeya kuelekea Makete? (Makofi)
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nimpongeze Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa sababu tumeshamlipa huyo mkandarasi ambaye alikuwa anasuasua. Tulikuwa na advance, lakini pia na certificate ambazo tumemlipa zote takribani shilingi bilioni tisa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Festo atakuwa shahidi kwamba eneo analotoka ni kati ya maeneo ambayo mvua inanyesha sana. Kwa hiyo, Mheshimiwa anafanya zile kazi za kujenga miundombinu mingine, lakini kwa maana ya barabara earthwork siyo rahisi kufanya kwa sasa hivi. Tayari tumeshamwagiza mkandarasi kwamba mvua inapopungua aingie site kwa sababu haidai Serikali, bali sisi tunamdai kazi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nimhakikishe Mheshimiwa Mbunge na wananchi wa Makete kwamba tumeshamlipa, tunamdai kazi, na tutahakikisha mvua tu inapokuwa imepungua, aanze kufanya kazi za kujenga barabara.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved