Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 3 Sitting 9 Works and Transport Wizara ya Ujenzi 96 2026-04-15

Name

Subira Khamis Mgalu

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. SUBIRA K. MGALU aliuliza: -

Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Barabara ya Tamko - Mapinga kwa kipande kilichosalia?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Subira Khamis Mgalu, Mbunge wa Bagamoyo, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ujenzi wa Barabara ya TAMCO – Mapinga unatekelezwa kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza inahusisha sehemu ya kuanzia NIDA hadi Pangani kilometa 3.8 na awamu ya pili inahusisha sehemu ya Pangani hadi Mapinga kilometa 14.62.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ujenzi wa barabara hii unatarajiwa kukamilika mwezi Juni, 2027. Aidha, Serikali inaahidi kuipa kipaumbele barabara hii kama sehemu ya kupunguza msongamano kwenye barabara kuu ya Dar es Salaam – Morogoro. Ahsante.