Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Janeth Peter Pinda

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. JANETH P. PINDA K.n.y. MHE. JESCA Y. MBOGO aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kufuatilia, kuboresha na kuweka uwazi katika utoaji wa mikopo ya asilimia 10, ili kuhakikisha inawafikia walengwa?

Supplementary Question 1

MHE. JANETH P. PINDA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana kwa kunipa nafasi ya nyongeza. Wanawake wengi wamekuwa wakiomba mikopo, lakini hawana elimu ya kutosha. Je, ni lini Serikali itatoa elimu kwa akinamama hawa ili waweze kupata elimu hiyo ya mikopo? Nashukuru sana.

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, moja ya vipaumbele vya utoaji wa mikopo ya 10% kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu ni kutoa elimu na hamasa kwa makundi husika. Serikali imeweka kamati katika ngazi za kata, wilaya na mkoa, lakini wapo Maafisa Maendeleo ya Jamii katika halmashauri zetu na kwa baadhi ya halmashauri mpaka kwenye ngazi ya kata.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba, bado kuna changamoto ya elimu na hamasa ya kutosha kwa makundi haya ambayo yanalengwa kwa ajili ya kupata mikopo ya 10%. Kwa hiyo, ninamhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba, Serikali itaendelea kuwasimamia watendaji wote katika ngazi za Mamlaka ya Serikali za Mitaa kuendelea kutoa elimu kwa akinamama, vijana na watu wenye ulemavu ili waweze kupata mikopo hii kwa kadiri inavyotakiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, trend ya mikopo hii inatia matumaini makubwa kwa sababu, tangu tuliporejesha utaratibu wa Julai, 2024, Serikali imekusanya jumla ya shilingi bilioni 253 kwa ajili ya kukopesha. Mpaka Disemba, 2025 tayari makundi haya yameshakopa shilingi bilioni 230.66 sawa na 91% ya malengo ya kukopesha kwa muda huo, lakini marejesho pia yameendelea kwenda vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kipindi hiki marejesho yaliyofanyika ndani ya muda ni shilingi bilioni 100.27 sawa na 82% ya malengo. Kwa hiyo, pamoja na changamoto za mikopo ya 10%, kuna matumaini na mtiririko au trend inayoonesha improvement kubwa. Serikali itaendelea kusimamia kuhakikisha mikopo hii inawafikia walengwa, lakini pia, urejeshaji unakuwa na ufanisi mkubwa zaidi.

Name

Athumin Omary Mapalilo

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. JANETH P. PINDA K.n.y. MHE. JESCA Y. MBOGO aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kufuatilia, kuboresha na kuweka uwazi katika utoaji wa mikopo ya asilimia 10, ili kuhakikisha inawafikia walengwa?

Supplementary Question 2

MHE. ATHUMIN O. MAPALILO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Kwa kuwa, mikopo hii ni muhimu sana kwa wananchi wetu, na walio wengi hawawezi kutumia mifumo hii ya ukopeshaji, hasa wale walioko kijijini, je, Serikali sasa haioni umuhimu wa kuwatumia Maafisa Watendaji wa Vijiji ili waweze kuwasaidia, hasa kundi la wanawake, kuweza kufikia fursa hizi za mikopo? (Makofi)

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Ni kweli, kama alivyosema Mheshimiwa Mbunge wa Viti Maalum, Mkoa wa Mtwara, kwamba Serikali inatambua changamoto hiyo, pamoja na kwamba, mfumo huu wa WEZESHA unatumika na simu yoyote; simu janja na simu za kawaida, lakini bado kuna changamoto ya uelewa kwa baadhi ya wanufaika au walengwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imeshatoa maelekezo kwamba, Watendaji wa Vijiji, Maafisa Maendeleo katika ngazi za kata na Maafisa Ustawi wa Jamii wawe sehemu ya kuwezesha kutoa elimu na hamasa kwa walengwa, ili waweze kupata elimu na ku-access mikopo hii kupitia maeneo yao. Kwa hiyo, suala hili linafanyika na tutaendelea kuliboresha zaidi ili watendaji waweze kuwasaidia vikundi hivi wapate nafuu na uwezo mzuri zaidi wa kupata mikopo hiyo.

Name

Happiness Daniel Ngwando

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. JANETH P. PINDA K.n.y. MHE. JESCA Y. MBOGO aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kufuatilia, kuboresha na kuweka uwazi katika utoaji wa mikopo ya asilimia 10, ili kuhakikisha inawafikia walengwa?

Supplementary Question 3

MHE. HAPPINESS D. NGWANDO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kuniona. Kwa kuwa, mfumo huu umewaathiri sana wanawake wa Mkoa wa Ruvuma, ile kwenda na kurudi kwa ajili ya kufuatilia kupata mkopo huu, kiasi kwamba, wametumia gharama zao, na biashara zao zimefilisika kwa vile ni biashara ndogo ndogo kama mbogamboga au mama lishe. Je, Serikali ina mpango gani wa kuwawezesha wamama hawa kupata fedha kwa haraka? Ahsante. (Makofi)

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imeendelea kuboresha mfumo wa mikopo hii ili kuanza kupunguza muda wa kusubiri, lakini pia, kuondoa gharama zisizokuwa na lazima na usumbufu kwa wajasiriamali wanaohitaji mikopo hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ninakubaliana na Mheshimiwa Mbunge kwamba, tunaendelea kuboresha. Moja ya mambo ambayo Serikali imetoa maelekezo, nitumie nafasi hii kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI kuwasisitiza Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kote nchini kwamba, vikundi vya wajasiriamali wanawake, vijana na watu wenye ulemavu mara baada ya kuwasilisha maombi yao, wapewe taarifa kwa njia ya simu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii itawafanya wasilazimike kusafiri kwenda na kurudi mara kwa mara, ili kuepuka gharama za nauli na gharama kubwa katika kuomba mikopo. Mikopo inapokuwa tayari wapewe taarifa kwa utaratibu wa uwazi kwa njia ya simu na mbao za matangazo, ili wananchi waweze kupata mikopo hiyo kwa wakati, na pia, bila kutumia gharama kubwa.

Name

Nyamizi Simon Mhoja

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. JANETH P. PINDA K.n.y. MHE. JESCA Y. MBOGO aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kufuatilia, kuboresha na kuweka uwazi katika utoaji wa mikopo ya asilimia 10, ili kuhakikisha inawafikia walengwa?

Supplementary Question 4

MHE. NYAMIZI S. MHOJA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kuniona. Nini mkakati wa Serikali kuwapa kipaumbele wanawake wenye watoto wenye ulemavu kupata mkopo huu wa 10%, kwani bado mpaka sasa wanapata ugumu wa kuifikia hii fursa ya 10%. Ahsante. (Makofi)

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, hoja hii ya akina mama au walezi wa watoto wenye ulemavu kupewa fursa ya kukopa mikopo hii, ili waweze kuwalea watoto wenye ulemavu imesemwa na Waheshimiwa Wabunge wengi katika michango hii inayoendelea, kama ambavyo Mheshimiwa Mbunge amesema. Sheria ya Mikopo ya 10% imepitishwa na Bunge lako Tukufu. Sheria ile inaeleza mikopo kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, na sio walezi wa watu wenye ulemavu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa ikiwa kuna sababu, Bunge lako Tukufu linaweza likaleta mapendekezo na kuipitia sheria hiyo, tukaiboresha kulingana na mazingira ambayo tunayaona. Serikali hii sikivu ipo tayari kufanya tathmini, na kuona jambo linalowezekana kwa manufaa ya watu ambao wamelengwa. (Makofi)

Name

Dr. Regina Christopher Malima

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. JANETH P. PINDA K.n.y. MHE. JESCA Y. MBOGO aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kufuatilia, kuboresha na kuweka uwazi katika utoaji wa mikopo ya asilimia 10, ili kuhakikisha inawafikia walengwa?

Supplementary Question 5

MHE. REGINA C. MALIMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kunipatia nafasi na mimi niweze kuuliza swali la nyongeza. Je, Serikali ina mkakati gani wa kuwaunganisha wahitimu wa vyuo vikuu na fursa za mikopo hii ya 10%, ili na wao waweze kujiajiri pindi wanapomaliza masomo yao? (Makofi)

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la Mbunge ni swali muhimu sana, lakini Serikali ilishaanza kutekeleza. Ninakumbuka miaka miwili iliyopita nilifanya ziara katika Halmashauri ya Nyamagana ambapo vijana wahitimu walijiunga pamoja, wakaanzisha kituo cha afya na wakapewa mkopo wa 10% na wakaendelea kuendesha kituo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia Dar es Salaam imefanya hivyo, wapo walimu ambao wamekopa, wamefungua tuition center na wanaendelea kufanya hivyo. Kwa hiyo, Serikali inawapatia fursa kupitia dirisha la mikopo ya 10% kwa vijana kupitia Halmashauri zao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitumie nafasi hii kuwahamasisha vijana wahitimu kote nchini kwamba waunde vikundi vyao, waende kuomba mikopo kwenye Halmashauri kulingana na taaluma zao, waanzishe shughuli zao kwa sababu dirisha lipo wazi kwa ajili yao, na lina faida kubwa kwa sababu wao wenyewe wanapata ajira, na pia wanaajiri vijana wengine katika maeneo hayo.

Name

Neema Peter Majule

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. JANETH P. PINDA K.n.y. MHE. JESCA Y. MBOGO aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kufuatilia, kuboresha na kuweka uwazi katika utoaji wa mikopo ya asilimia 10, ili kuhakikisha inawafikia walengwa?

Supplementary Question 6

MHE. DKT. NEEMA P. MAJULE: Mheshimiwa Mwenyekiti, suala hili la watu wenye ulemavu linapigiwa kelele sana kwa sababu ya ukubwa wa tatizo hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika nchi yetu population ya walemavu inazidi kukua hasa baada ya ajali nyingi za bodaboda na vitu vingine. Je, Serikali haiwezi ikahama kufikiria kuhusu mikopo ya kuwawezesha wananchi wake, ikaenda sasa hata kufikiria ruzuku ili hawa wanawake ambao wana ulemavu waweze kupewa ruzuku, kwa maana hata muda wa kufanya hizo biashara hawana. Ahsante. (Makofi)

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ninamshukuru Mheshimiwa Dkt. Neema kwa wazo zuri na ushauri mzuri kwa Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sasa watu wenye ulemavu wananufaika kupitia asilimia mbili, na ukiangalia trend ya mikopo hiyo kwa kiasi kikubwa fedha zile zimekuwa zinawatosheleza kwa sababu waombaji hawajawa wengi, lakini tunajua kuna gap ya elimu. Tunaendelea kuwaelimisha na kuhamasisha watu wenye ulemavu wapate hiyo mikopo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wazo la ruzuku tumelipokea kama Serikali, tutalifanyia tathmini na kuona namna nzuri ya kwenda nalo. (Makofi)

Name

Edwin Enosy Swalle

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Lupembe

Primary Question

MHE. JANETH P. PINDA K.n.y. MHE. JESCA Y. MBOGO aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kufuatilia, kuboresha na kuweka uwazi katika utoaji wa mikopo ya asilimia 10, ili kuhakikisha inawafikia walengwa?

Supplementary Question 7

MHE. EDWIN E. SWALLE: Mheshimiwa Mwenyekiti, Sheria ya Mikopo ya 10% imetoa fursa kwa watu wenye ulemavu kukopa mtu mmoja mmoja; pia imetoa fursa kwa watu kuunda vikundi vya watu watano na kuendelea, lakini wapo vijana wengi wamehitimu vyuo vikuu na vyuo vya kati wana ujuzi maalum ambao pengine kuwapata kuwa kikundi, watu wengi ni ngumu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, je, Serikali haioni haja sasa kuongeza kundi la nne ambalo ni la watu ambao wana ujuzi maalum waruhusiwe kukopa mtu mmoja, mmoja? Ahsante.

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ninamshukuru sana Mheshimiwa Edwin Enosy Swalle, Mbunge wa Lupembe kwa wazo zuri. Serikali ipo tayari kupokea mawazo ya Waheshimiwa Wabunge. Kupitia wataalam wetu watakaa na kufanya tathmini, na tutapata majibu na kuona namna ya kuzingatia ushauri huo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tunapokea ushauri huo wa Mheshimiwa Mbunge na tutafanya tathmini kupitia taratibu za Serikali na kuona namna ya kuboresha hatua kwa hatua, kwa sababu mikopo hii itaendelea kuboreshwa siku hadi siku kulingana na mahitaji ya jamii yetu. Ahsante sana.

Name

Khadija Shaaban Taya

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. JANETH P. PINDA K.n.y. MHE. JESCA Y. MBOGO aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kufuatilia, kuboresha na kuweka uwazi katika utoaji wa mikopo ya asilimia 10, ili kuhakikisha inawafikia walengwa?

Supplementary Question 8

MHE. KHADIJA S. TAYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa, kuna fursa ya 30% ya manunuzi na imemtaja mtu mwenye ulemavu kama mnufaika, je, Serikali haioni haja ya kusisitiza katika kila Halmashauri Tanzania kuweza kuhakikisha sheria ile inatekelezwa kiuhakika ili kuweza kumnufaisha mtu mwenye ulemavu? Ninashukuru.

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kama alivyosema Mheshimiwa Khadija au Keisha Mbunge wa Viti Maalum kwamba kupitia sheria za PPRA 30% ya shughuli za zabuni zinatakiwa kukopeshwa kwa makundi maalum ambayo ni wanawake na watu wenye ulemavu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala hili limeendelea kutekelezwa, lakini bado mwamko na elimu haujawa wa kutosha. Kwa hiyo, ninaomba nimhakikishie Mbunge kwamba, Serikali na Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI kwa kushirikiana na PPRA, Wizara ya Fedha na Wizara nyingine kama ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, tunaendelea kuhamasisha kuhakikisha fursa hiyo inatumika ipasavyo na makundi ya watu wenye ulemavu wananufaika na mpango huu mzuri wa Serikali.

Name

Stella Ikupa Alex

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. JANETH P. PINDA K.n.y. MHE. JESCA Y. MBOGO aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kufuatilia, kuboresha na kuweka uwazi katika utoaji wa mikopo ya asilimia 10, ili kuhakikisha inawafikia walengwa?

Supplementary Question 9

MHE. STELLA I. ALEX: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na Serikali kutoa mwongozo kwamba mtu mwenye ulemavu mmoja mmoja aruhusiwe kukopesheka, lakini hili halitekelezeki kwenye Manispaa na Halmashauri zetu. Je, ni nini kauli ya Serikali kwa hili?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mujibu wa sheria na kanuni za mikopo ya 10% watu wenye ulemavu wanayo fursa ya kukopa mtu mmoja, mmoja, na huo ndiyo msimamo wa Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba kama kuna eneo lolote Halmashauri yoyote ambayo mikopo ya asilimia mbili kwa watu wenye ulemavu ina mkwamo wowote kwa wanaohitaji na wenye sifa, tupate taarifa hizo, tuweze kulifanyia kazi ili kuhakikisha watu wote wenye ulemavu ambao wanahitaji kupata mikopo hiyo wanapata kwa mujibu wa sheria na kanuni zilivyowekwa.