Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 3 Sitting 9 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Waziri Mkuu-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) 90 2026-04-15

Name

Jesca Yuda Mbogo

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. JANETH P. PINDA K.n.y. MHE. JESCA Y. MBOGO aliuliza:-

Je, Serikali ina mpango gani wa kufuatilia, kuboresha na kuweka uwazi katika utoaji wa mikopo ya asilimia 10, ili kuhakikisha inawafikia walengwa?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Jesca Yusa Mbogo, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kutatua changamoto zilizokuwepo katika utekelezaji wa utoaji wa mikopo ya asilimia 10, zikiwemo changamoto za ufuatiliaji, uwazi na kuhakikisha mikopo inawafikia walengwa kuanzia mwaka 2024/2025, Serikali imefanya maboresho ya kimfumo yaliyojikita katika kuimarisha utoaji, usimamizi na ufuatiliaji wa mikopo kwa kutumia teknolojia, kuboresha uwezo wa walengwa kupitia mafunzo, kuongeza uwazi kwa kutumia mfumo wa kielektroniki katika kuomba, kutoa, na kusimamia shughuli zinazotekelezwa na kufuatilia marejesho.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hatua zilizochukuliwa ni pamoja na kuanzisha mfumo wa kidigitali wa WEZESHA unaowawezesha wateja kuomba mikopo, kuchakata, kutoa mikopo, kufuatilia shughuli zinazotekelezwa na urejeshaji. Suala hili limeongeza uwazi, uwajibikaji na utunzaji wa kumbukumbu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, utaratibu wa kutumia mabenki katika ukopeshaji na usimamizi wa mikopo hii pia, umeanza katika halmashauri 10 za mfano ambapo pia, mfumo wa kibenki umeunganishwa na mfumo wa WEZESHA wa Halmashauri.