Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Miraji Jumanne Mtaturu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Singida Mashariki

Primary Question

MHE. MIRAJI J. MTATURU aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga majosho ya kuogeshea mifugo kwenye vijiji vya Jimbo la Singida Mashariki?

Supplementary Question 1

MHE. MIRAJI J. MTATURU: Mheshimiwa Spika, ahsante sana na namshukuru sana Mheshimiwa Waziri kwa majibu mazuri, lakini pamoja na hayo nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, swali la kwanza, tunaishukuru Serikali kwa kutupatia fedha katika Kijiji cha Ntuntu tumeweza kujengewa josho na linafanya kazi tunashukuru sana, lakini katika Kijiji cha Siuyu tulikuwa na changamoto kubwa ya mgogoro, lile josho lilikuwa limejengwa kwenye maeneo ya Kanisa la RC pale Siuyu, tukawa tumeomba Serikali lihamishwe na eneo lipo tayari. Ni mwaka wa tatu sasa tumeahidiwa halijakamilika. Ni lini sasa Serikali itajenga josho katika Kijiji cha Siuyu ili kuondokana na changamoto ambayo ipo ikiwemo kuondoa mgogoro uliopo kati ya kanisa na wananchi? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili, ni kwamba katika Jimbo la Singida Mashariki ambalo sasa ni Ikungi Mashariki tuna mifugo mingi sana maeneo ya Isuna, Ng’ongosolo, Ulyampiti, Mang’onyi, Msule na Choda, ni lini sasa majosho yatajengwa kwa ajili ya afya ya mifugo ya wananchi ambayo ni uchumi mkubwa katika eneo hilo? (Makofi)

Name

Alexander Pastory Mnyeti

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Misungwi

Answer

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Spika, nianze na hili la josho lililojengwa kwenye eneo la kanisa, tutatuma wataalamu kutoka Wizara ya Mifugo, kwenda kuangalia eneo hilo limekaaje na kisha tutachukua hatua ya kuhamisha josho hilo kupeleka kwenye maeneo ambayo wananchi watapendekeza, lakini hili la pili la wingi wa mifugo katika jimbo la Mheshimiwa Mtaturu, tutatuma wataalamu pia kwenda kuangalia idadi ya mifugo iliyopo hapo na uwezeshaji wa majosho yetu kama yanatosha kukidhi haja ya mifugo iliyopo hapo.

Kwa hiyo, tukishaona kuna umuhimu wa kujenga majosho mengine tupo tayari kupeleka majosho katika jimbo hilo, ahsante.

Name

Lucy John Sabu

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MIRAJI J. MTATURU aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga majosho ya kuogeshea mifugo kwenye vijiji vya Jimbo la Singida Mashariki?

Supplementary Question 2

MHE. LUCY J. SABU: Mheshimiwa Spika, je, Serikali ina mpango gani wa kujenga majosho katika maeneo ya pembezoni mwa Mji wa Bariadi? Ahsante. (Makofi)

Name

Alexander Pastory Mnyeti

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Misungwi

Answer

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Spika, ahsante, labda nimuombe Mheshimiwa Mbunge baada ya Bunge hili tutatuma wataalamu kwenda kuangalia umuhimu wa kujenga majosho katika maeneo hayo kulingana na wingi wa mifugo inayopatikana katika pembezoni mwa Mji wa Bariadi, lakini pia niiombe Halmashauri ya Mji wa Bariadi kuona umuhimu wa kuwajengea majosho wafugaji wetu katika maeneo haya yanayozunguka kwa sababu mifugo hawa wanaingiza kipato ndani ya halmashauri, lakini pia Serikali Kuu. Kwa hiyo, tutatuma wataalamu kwenda kuangalia kama kuna umuhimu wa kuongeza majosho katika maeneo hayo.

Name

Francis Kumba Ndulane

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilwa Kaskazini

Primary Question

MHE. MIRAJI J. MTATURU aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga majosho ya kuogeshea mifugo kwenye vijiji vya Jimbo la Singida Mashariki?

Supplementary Question 3

MHE. FRANCIS K. NDULANE: Mheshimiwa Spika, je, Serikali ina mpango gani wa kujenga majosho na malambo katika vijiji 90 vya Wilaya ya Kilwa? (Makofi)

Name

Alexander Pastory Mnyeti

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Misungwi

Answer

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Spika, kama nilivyosema katika jibu la msingi kwamba Serikali inaendelea kujenga majosho, lakini pia na malambo katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu kulingana na umuhimu na mahitaji ya wafugaji wetu wanaopatikana katika maeneo hayo. Kwa hiyo, kama kuna mahitaji ya wafugaji wetu katika jimbo lake Mheshimiwa Mbunge, tupo tayari kujenga maeneo hayo kulingana na upatikanaji wa fedha kadiri ambavyo inawezekana, ahsante. (Makofi)

Name

Charles Muguta Kajege

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mwibara

Primary Question

MHE. MIRAJI J. MTATURU aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga majosho ya kuogeshea mifugo kwenye vijiji vya Jimbo la Singida Mashariki?

Supplementary Question 4

MHE. CHARLES M. KAJEGE: Mheshimiwa Spika, ufugaji ni mojawapo ya sekta muhimu sana za uchumi katika Jimbo la Mwibara, je, ni lini Serikali itajenga majosho katika Kata za Namhula, Igundu, Nansimo, Iramba na Kasuguti?

Name

Alexander Pastory Mnyeti

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Misungwi

Answer

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Spika, tutatuma wataalamu kwenye Jimbo la Mwibara kwenda kuangalia umuhimu wa kujenga majosho hayo, lakini pia kwa taarifa tulizonazo ni kwamba tayari kwenye jimbo la Mheshimiwa Mbunge tuna majosho zaidi ya matatu ambayo tumeyajenga kupitia bajeti iliyopita. Kwa hiyo, tutaendelea kuboresha, tutaendelea kuongeza majosho katika jimbo la Mheshimiwa na hakika mambo yatakwenda vizuri, ahsante.

Name

Eng. Stella Martin Manyanya

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Nyasa

Primary Question

MHE. MIRAJI J. MTATURU aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga majosho ya kuogeshea mifugo kwenye vijiji vya Jimbo la Singida Mashariki?

Supplementary Question 5

MHE. ENG. STELLA M. MANYANYA: Mheshimiwa Spika, ahsante, kwa nini Serikali hasa Wizara yako imezingatia zaidi ujenzi wa majosho na kutelekeza ujenzi wa mialo kama ilivyotelekeza katika Mwalo wa Ng’ombo kiasi cha mkandarasi kuondoka? (Makofi)

Name

Alexander Pastory Mnyeti

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Misungwi

Answer

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Spika, si kweli kwamba Serikali imetelekeza huo mwalo, isipokuwa kilichotokea ni kwamba ni uhaba wa fedha, mara tu tutakapopata fedha tutamlipa mkandarasi huyo na atarudi site kwenda kukamilisha kazi ambayo amekwisha ianza, ahsante.