Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 26 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Waziri wa Mifugo na Uvuvi 338 2025-05-16

Name

Miraji Jumanne Mtaturu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Singida Mashariki

Primary Question

MHE. MIRAJI J. MTATURU aliuliza: -

Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga majosho ya kuogeshea mifugo kwenye vijiji vya Jimbo la Singida Mashariki?

Name

Alexander Pastory Mnyeti

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Misungwi

Answer

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI alijibu: -
Mheshimiwa Spika, katika bajeti ya mwaka 2022/2023 Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi ilitumia kiasi cha shilingi milioni 92 kwa ajili ya kujenga majosho manne katika Halmashauri ya Ikungi linapopatikana Jimbo la Singida Mashariki ambapo kupitia fedha hizo Jimbo la Singida Mashariki lilifanikiwa kujengewa josho moja lililopo katika Kijiji cha Ntuntu lenye thamani ya shilingi milioni 23. Josho hilo limekamilika kwa 100% na linafanya kazi. Aidha, Wizara inaendelea kuratibu ujenzi wa majosho katika maeneo mbalimbali hapa nchini ikiwemo vijiji vya Jimbo la Singida Mashariki kadiri ya upatikanaji wa fedha.

Mheshimiwa Spika, aidha, Wizara inashauri Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi inayosimamia Jimbo la Singida Mashariki kutenga fedha kutoka katika mapato yao ya ndani kwa ajili ya ujenzi wa majosho katika jimbo hilo kwa lengo la kudhibiti magonjwa yaenezwayo na kupe, mbung’o na wadudu wengine, ahsante.