Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Ali Juma Mohamed

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Shaurimoyo

Primary Question

MHE. ALI JUMA MOHAMED aliuliza: - Je, kwa nini michango ya Bima ya Afya isiwe sawa na utaratibu wa michango ya pensheni kati ya mwajiri na mtumishi?

Supplementary Question 1

MHE. ALI JUMA MOHAMED: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, nilikuwa na swali moja la nyongeza.

Je, ni kwa kiasi gani NHIF huwa inachukua hatua kwa changamoto mbalimbali ambazo huwa zinajitokeza katika hospitali mbalimbali hapa nchini juu ya wanachama wake? (Makofi)

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, nijibu swali la kaka yangu analosema kwamba ni kwa kiwango gani ina react Bima ya Afya, inapotokea changamoto mbalimbali za Bima ya Afya kwa wanachama wake.

Mheshimiwa Spika, kwa kweli Bima ya Afya, imekuwa iki-react kulingana na matatizo yenyewe yanavyokuja na aina ya tatizo. Nikuhakikishie pia ni kweli kwamba hapa karibuni pamekuwa na malalamiko mengi sana kwa wateja, lakini pili, kwa kutoka maeneo mbalimbali kuhusiana na bima.

Mheshimiwa Spika, mimi ninachotaka kumtoa Mheshimiwa Mbunge, wasiwasi kila wakati na wewe unajua sasa hivi tuna Mkurugenzi wa Bima ya Afya, dada yetu ambaye ana experience kubwa, exposure kubwa na ni mzuri sana kwenye kutatua matatizo. Nikuondoe wasiwasi Mheshimiwa Mbunge kuwa matatizo ya nyuma uliyokuwa unayasikia kwa aina ya Mkurugenzi tuliyenaye sasa hivi nataka kukuhakikishia yanatatuliwa kwa wakati na yanasimamiwa kwa uadilifu mkubwa sana. (Makofi)

Name

Fatma Hassan Toufiq

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ALI JUMA MOHAMED aliuliza: - Je, kwa nini michango ya Bima ya Afya isiwe sawa na utaratibu wa michango ya pensheni kati ya mwajiri na mtumishi?

Supplementary Question 2

MHE. FATMA H. TOUFIQ: Mheshimiwa Spika, kwa kuwa watumishi wa Serikali, wanapostaafu wanaendelea kupata huduma ya Bima ya Afya, je, upi utaratibu wa wazazi wa wale watumishi waliostaafu kuendelea kupata huduma ya Bima ya Afya?

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, utaratibu wa kuwahudumia wazazi wa waliostaafu ambao mimi naamini watakuwa ni wachache sana, naomba tu niseme kwamba kwa sababu kama kumeibuka matatizo kama hayo kwa wakati huu, nimuombe Mheshimiwa, kwa sababu ni Mjumbe wa Kamati kwenye suala zima la Bima ya Afya kwa wote ambalo tunaelekea huko mbele, nafikiri ni moja wapo ya mchango mzuri ambao unaweza ukajadiliwa na kuona tunafanyaje kuhakikisha eneo hilo linaweza kuwa covered bila kuathiri mambo mengine ya kibajeti inapotokea masuala ya uendeshaji wa mfuko.