Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
George Ranwell Mwenisongole
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mbozi
Primary Question
MHE. GEORGE R. MWENISONGOLE aliuliza:- Je, Sera ya Taifa ya Afya ya mwaka 2007 inayosema akina mama wajawazito watajifungua bure bila malipo bado ipo?
Supplementary Question 1
MHE. GEORGE R. MWENISONGOLE: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali ya nyongeza. Kwanza nishukuru kwamba Serikali imekiri kwamba hii sera ipo lakini kiuhalisia hakuna mama yeyote mjamzito hapa Tanzania anayejifungua bure.
Sasa nini kauli ya Serikali yakuzitaka hizi zahanati, vituo vya afya na hospitali ambazo zinatoza akina mama wajawazito kinyume na sera yetu ya mwaka 2007?
Swali la pili, sasa hivi mama akienda kujifungua anaambiwa lete nyuzi, lete dripu, lete gloves na hivyo vifaa sio vyote vinavyotumika na vikibaki vinabaki kule hospitali. Sasa nini kauli ya Serikali kuhakikisha hilo jambo haliendelei? Ahsante. (Makofi)
Name
Dr. Godwin Oloyce Mollel
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Siha
Answer
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, kwanza nimtoe wasiwasi Mheshimiwa Mbunge kwamba hii sera hai-apply, ni kweli ina-apply lakini kwa sababu ukiangalia na ukipiga hesabu ili uweze kuwahudumia wakina mama wote bure kama ambavyo Mheshimiwa Mbunge, ametamani unahitaji shilingi bilioni 227. Ukweli hapa Bungeni ninyi mnajua wenyewe kwamba tumekuwa tukitenga shilingi bilioni 200 kwa ajili ya dawa tu, maana yake ni nini? Ni ukweli kwamba hutaweza kuwahudumia kina mama wote kwa bure kama ambavyo ametamani Mheshimiwa Mbunge.
SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, vifaa vinavyobaki anavyokuwa ameleta mama kujifungua, ndio lilikuwa swali lake la pili. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, vifaa vinavyobaki ndio hayo hayo inarudi pale pale kwamba tunahitaji kujua specifically eneo husika, kwa sababu kama unamwambia mtu kuna vifaa vyake vinabaki, lakini mwisho wa siku zikibaki ni zinakwenda wapi, ndio hayo bado tunasema kunawezekana kuna tatizo kwenye leadership, kwa sababu tulivyokwenda kwenye jimbo lake, tulikwenda tukakuta kwanza, tulikutana na nilisema lete hii inaitwa slip ya benki, lakini wakaleta slip ya benki moja ambayo mwisho wa siku tuliikuta imekuwa-forged, lakini mwisho wa siku tunakwenda tunakuta wana shilingi milioni zaidi ya 300, tukakutana na mambo mengi mabovu mabovu.
Mheshimiwa Spika, kwa maana hiyo wakati mwingine kuna mambo mengine yanatokea ni ya uongozi na mengine ni nje ya uwezo wa muhusika aliyopo pale. Kwa hiyo, kila jambo ninatamani tuli-deal kwa kuangalia tatizo limetokea wapi ili tuweze kuhukumu kwa haki. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, lakini Mheshimiwa Mbunge, akumbuke tulikwenda ziara ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, pamoja na wewe jimboni kwako, unakumbuka mimi na wewe Mheshimiwa Waziri Mkuu, alivyotuacha tulienda pamoja kwenye kituo cha afya kilicholalamikiwa, lakini hospitali ya wilaya, ulikuta kwamba walikosea kwenye kutengeneza maoteo. Maana yake tulikuta kwamba matumizi yao ya mwaka ni zaidi ya shilingi milioni 800 lakini wao wakaleta matumizi ya shilingi milioni 400 na wakati huo tayari wameshatumia shilingi milioni 507.
Mheshimiwa Spika, maana yake ni nini? Kuna shida katika eneo la uongozi na kama unakumbuka tulienda kwa DMO tukakuta bado kuna zaidi ya shilingi milioni 400 kwenye akaunti hazitumiki, lakini hospitali haina dawa.
Kwa hiyo matatizo kama hayo ya uongozi yanaweza yakawa yanaleta shida, kwa hiyo, mimi nikuombe Mheshimiwa Mbunge, tuwasiliane ili tuweze kuliangalia kila jambo specifically ili tuli-treat kama linavyowezekana kwa sababu mengine yanawezekana yakawa ni ya kibajeti kweli kwamba wamemaliza hawana lakini mengine yanaweza yakatokana ni namna leadership wanavyofanya wenyewe. (Makofi)
Name
Condester Michael Sichalwe
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Momba
Primary Question
MHE. GEORGE R. MWENISONGOLE aliuliza:- Je, Sera ya Taifa ya Afya ya mwaka 2007 inayosema akina mama wajawazito watajifungua bure bila malipo bado ipo?
Supplementary Question 2
MHE. CONDESTER M. SICHALWE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa nafasi. Pamoja na kuwa na sera nyingi, ipo pia sera ya watoto chini ya miaka mitano, kutibiwa bure na sera hii haijawahi kutekelezeka hata kidogo. Katika majibu ya msingi ya Naibu Waziri, yanasema ametoa takwimu ya wamama wajawazito, kwamba wakiwahudumia wote haitawezekana...
SPIKA: Mheshimiwa uliza swali.
MHE. CONDESTER M. SICHALWE: Mheshimiwa Spika, swali, sasa kama takwimu ya watu wanaopaswa kuhudumiwa ni wengi, watoto na akina mama wajawazito, kwa nini Serikali isitoke kuwaambia wananchi kwamba sera hizi hazipo ili waelewe kwamba hakuna bure kwa wajawazito wala hakuna bure kwa watoto chini ya miaka mitano? (Makofi)
Name
Dr. Godwin Oloyce Mollel
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Siha
Answer
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, labda tu nimwambie Mbunge namuelewa sana, ila hata yeye kwenye mipango yake ambayo ameipanga, anaianza anapanga mpango mzima, lakini anautekeleza hatua kwa hatua na nimwambie tu kwa maana ya exemption, kwa maana watu waliotibiwa na yeye mwenyewe anajua jinsi tumepambana na yeye kwenye hospitali yake ya rufaa kule Mbeya, kwa maana ya watu wa exemption kwa mwaka tu Serikali inatumia zaidi ya shilingi bilioni 667, lakini ukweli ukikuta waliohitaji exemption ni zaidi ya hao lakini pasingekuwepo na hiyo sheria pia hawa tuliyowasaidia shilingi bilioni 667 pasingekuwepo na namna ya kutekeleza.
Kwa hiyo, sheria ipo ila ni ukweli kwamba haijatekelezwa kwa 100% lakini siku zote unaweza ukapanga mipango, lakini bajeti ya kutekeleza kwa 100% inaweza isipatikane lakini ukitekeleza kwa 60% nayo ni utekelezaji, ni kujipanga kumalizia 40%. (Makofi)
Name
Luhaga Joelson Mpina
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kisesa
Primary Question
MHE. GEORGE R. MWENISONGOLE aliuliza:- Je, Sera ya Taifa ya Afya ya mwaka 2007 inayosema akina mama wajawazito watajifungua bure bila malipo bado ipo?
Supplementary Question 3
MHE. LUHAGA J. MPINA: Mheshimiwa Spika, kwa kuwa fedha ya Serikali inatozwa kwa mujibu wa sera na kwa mujibu wa sheria; je, utolewaji wa huduma za afya zilipata wapi mamlaka ya kuwatoza hawa akina mama wajawazito pamoja na watoto wenye umri chini ya miaka mitano huku ikijua kabisa kwamba kasma ile haipo kwa mujibu wa sheria wala sera hairuhusu, waliruhusiwa na nani kufanya hayo? (Kicheko)
Name
Dr. Godwin Oloyce Mollel
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Siha
Answer
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, nijaribu tu kumwambia Mpina, kuna sheria, kanuni lakini pia wakati...
SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, ni Mheshimiwa Mpina.
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, okay, naomba nimjibu kaka yangu Mheshimiwa Mpina, kwa kumwambia wakati mwingine katika sheria, kuna wakati kuna sheria iliyopo, kuna kanuni zilizopo, lakini pia kuna kutumia busara. Maana yake sisi tuna bajeti ya shilingi bilioni 200 kwa ajili ya dawa na vitendanishi, lakini matumizi ni zaidi ya hiyo. Kwa hiyo, anapokuja mgonjwa tunatumia hekima na busara yule anayeweza kulipa analipa, asiyeweza kulipa anahudumiwa na sheria iliyopo.
Kwa hiyo, kwa busara hiyo ndio maana yeye yupo salama, wananchi waliyopo kwenye jimbo lake wapo salama na leo Tanzania ina afya. (Makofi)
Name
Felista Deogratius Njau
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. GEORGE R. MWENISONGOLE aliuliza:- Je, Sera ya Taifa ya Afya ya mwaka 2007 inayosema akina mama wajawazito watajifungua bure bila malipo bado ipo?
Supplementary Question 4
MHE. FELISTA D. NJAU: Mheshimiwa Spika, ahsante, nakushukuru kunipa niulize swali dogo la nyongeza.
Mheshimiwa Spika, pamoja na wakina Mama, kubeba delivery kit kuelekea katika hospitali wakati wa kujifungua hasa vijijini, wakienda wakakutana na changamoto ambayo wanatakiwa wafanyiwe operation, wanatakiwa walipe kwanza pesa ya operation ndio wafanyiwe operation na hii inapelekea akina mama wengi kufa wakati wa uzazi; nini kauli ya Serikali katika hili? (Makofi)
Name
Dr. Godwin Oloyce Mollel
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Siha
Answer
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, kauli ya Serikali kwenye eneo hilo ni msimamo wa Dkt. Samia Suluhu Hassan, alipolihutubia Bunge hili kwa mara ya kwanza, alipofika eneo la huduma ya mama na mtoto alirudia mara mbili na akaongea kwa msisitizo mkubwa na ndio maana unaona baada ya yeye kutoka hapa Bungeni, alidumbukiza resources sekta ya afya na ndio maana leo tuna nishani kwenye eneo hilo la kina mama na watoto, ukilinganisha na duniani, tuna nishani ya kidunia ambayo Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kati ya Marais saba duniani waliyopata nishani yumo lakini kwa Afrika ni Rais pekee aliyepata.
Mheshimiwa Spika, sasa ni kweli hayo yanayotokea, tamko la Serikali Mtanzania yeyote siyo tu mama mjamzito, akifika kwenye kituo cha afya ni lazima cha kwanza ni kuokoa maisha na kuhakikisha huyo mtu salama, ndio mambo mengine yafuate. Kwa hiyo, akipatikana mtu ambaye anasababisha kitokee kifo kwa sababu alikuwa anasubiri fedha hata kwa maadili yetu unanyang’anywa cheti na hautaruhusiwa tena ku-practise. (Makofi)