Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Bernadeta Kasabago Mushashu

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. BENARDETA K. MUSHASHU aliuliza:- Je, kuna mpango gani kuhakikisha sekta zote zinashiriki vita dhidi ya magonjwa yasiyoambukiza yanayosababisha vifo vingi nchini?

Supplementary Question 1

MHE. BENARDETA K. MUSHASHU: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri ya Naibu Waziri nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, zaidi ya 33% ya vifo vinavyotokea hapa nchini vinasababishwa na magonjwa yasiyoambukiza kama kisukari, pressure, magonjwa mbalimbali ya moyo na kadhalika. Je, nia afua gani hasa zinazotekelezwa ndani ya Tanzania ili wananchi wote wajue namna ya kujikinga? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili, kwa kuwa matibabu ya magonjwa haya yanachukua muda mrefu kawaida ukiugua ni maisha yako yote na unakuwa unatumia dawa kwa hiyo nigare lakini kwa kuwa magonjwa haya yanaweza kuzuilika; je, kwa nini Serikali isiwekeze zaidi ikaweka mikakati mikubwa, bajeti kubwa katika kuzuia kuliko kungoja kuja kutibu? (Makofi)

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Mbunge na kwanza nimpongeze tu kama kiongozi katika Kamati inayosimamia afya kwa kweli imekuwa ni eneo lake zuri sana ambalo amekuwa akilipigania wakati wowote na kulisemea.

Mheshimiwa Spika, niseme tu swali lake la kwanza ni afua zipi? Moja kwa kweli wewe mwenyewe umeona jinsi hata Bunge hili linavyosisitiza masuala ya kufanya mazoezi na kuishi maisha yenye afya na masuala ya lishe na wakati wote mmeona vyombo vya habari vikifanya hivyo.

Mheshimiwa Spika, lakini anajua tunasema hapa Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan amewekeza kwenye sekta ya afya zaidi ya shilingi trilioni 6.7 ambazo tu hazijaleta mapinduzi kwenye sekta ya afya ndani ya nchi lakini unaona sasa nchi zilizotuzunguka wanakuja kupata huduma ndani ya Tanzania. Ukiangalia vifaa vile ambavyo mimi na wewe tumekuwa tukitembea kwenye hospitali zetu za Mikoa, Taifa utaona asilimia kubwa ya hivyo vifaa vimekuja kutatua matatizo yanayotokana na tatizo ulilolizungumzia hapa. Kwa hiyo, moja; bajeti imetengwa vizuri lakini kwa kweli Serikali imezingatia kwenye eneo hilo.

Mheshimiwa Spika, la pili kwa nini isiongezwe bajeti kwenye eneo hilo? Mheshimiwa Mbunge mimi nikuhakikishie inafanyika kikubwa sana kwenye eneo hilo ndiyo maana umeona miundombinu hata kwa mwaka 2022/2024 utaona jinsi ambavyo teknolojia imenunuliwa lakini umeona jinsi ambavyo miundombinu imejegwa kuanzia ngazi ya zahanati mpaka ngazi ya Taifa kuhakikisha tunawagundua watu kama hao mapema kabla ya magonjwa hayajafika mbali. (Makofi)

Name

Prof. Patrick Alois Ndakidemi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Moshi Vijijini

Primary Question

MHE. BENARDETA K. MUSHASHU aliuliza:- Je, kuna mpango gani kuhakikisha sekta zote zinashiriki vita dhidi ya magonjwa yasiyoambukiza yanayosababisha vifo vingi nchini?

Supplementary Question 2

MHE. PROF. PATRICK A. NDAKIDEMI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza na nianze kwa kuipongeza Serikali kwa jinsi inavyopambana na ugonjwa wa selimundu kwa sababu ugonjwa huu unaenea sana Ukanda wa Ziwa, Kati na maeneo mengine nchini. Sasa gharama za kutibu ugonjwa huu ni kubwa sana Serikali ina mpango gani kuhakikisha wananchi wanatibiwa bure kwa sababu gharama ni kubwa na wananchi wengi hawawezi kumudu hizi gharama? Ahsante sana. (Makofi)

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, kwanza nimjibu Mbunge bingwa wa Moshi Vijijini ambapo toka Moshi Vijijini ianzishwe haijapata mtetezi mzuri kama huyu hapa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, niseme tu kwamba selimundu kama ambavyo mnajua ni moja wapo wa uwekezaji ambao Rais wetu amewekeza kwenye nchi yetu kwa kiasi kikubwa na kama mnakumbuka miaka miwili iliyopita ukipata selimundu kinachokutokea ni kwamba tatizo linakusumbua na watu wengi hawafikishi miaka 45 anakuwa amekufa.

Mheshimiwa Spika, lakini Rais wetu ametuletea teknolojia na mnakumbuka tulivyokuja kwenye bajeti yetu ya mwaka jana uliona mtoto aliyeletwa hapa ambaye tayari ametibiwa ndani ya nchi hii na akapona selimundu na mpaka sasa watoto zaidi ya 30 wametibiwa na wote wametibiwa bure.

Waheshimiwa Wabunge, niwaombe tunapoelekea sasa kwenye Bima ya Afya kwa Wote nadhani ndiyo itakuwa suluhisho la kudumu kwa sababu sasa hivi hawa wanaotibiwa bure siyo kutoka kwenye bajeti ya Taifa ni juhudi za Rais binafsi kutafuta fedha kwa wadau na kusaidia hao maskini wasiyojiweza. (Makofi)

Name

Dr. Christina Christopher Mnzava

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. BENARDETA K. MUSHASHU aliuliza:- Je, kuna mpango gani kuhakikisha sekta zote zinashiriki vita dhidi ya magonjwa yasiyoambukiza yanayosababisha vifo vingi nchini?

Supplementary Question 3

MHE. DKT. CHRISTINA C. MNZAVA: Mheshimiwa Spika, kwa kuwa sababu moja wapo ya magonjwa yasiyoambukiza ni suala zima la mfumo wa chakula, namna ya ulaji wa chakula na kulikuwa na taasisi ambayo ilikuwa inashughulikia masuala ya chakula na lishe, ikarudishwa kwenye Wizara ya Afya; je, hamuoni sasa kuna umuhimu wa Taasisi ya Chakula na Lishe kusimama yenyewe kama taasisi ili iweze kufanya utafiti? (Makofi)

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, ninakubaliana kabisa na Mheshimiwa Dkt. Mnzava kwamba masuala haya ukitaka kuyaondoa na kuyapunguza kabisa una-deal na eneo la lishe, lakini kuna mchakato maalumu uliofanywa na Serikali, ushauri na michakato mbalimbali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ndiyo maamuzi yaliyofanyika yakafanyika. Ninachotoka kumuhakikishia hii Taasisi ya Lishe inakuja ndani ya Wizara na kuwa kama Idara na Waziri wetu ataisimamia kwa karibu sana na kuhakikisha inaleta matokeo makubwa hata kuliko ilivyokuwa inajisimamia yenyewe.

Name

Grace Victor Tendega

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. BENARDETA K. MUSHASHU aliuliza:- Je, kuna mpango gani kuhakikisha sekta zote zinashiriki vita dhidi ya magonjwa yasiyoambukiza yanayosababisha vifo vingi nchini?

Supplementary Question 4

MHE. GRACE V. TENDEGA: Mheshimiwa Spika, kwa nini Wizara ya Afya isije na mpango mkakati kushirikiana na Wizara ya Michezo na Wizara ya Ujenzi kuhakikisha kwamba kunajengwa viwanja na ili wananchi waweze kuweza kukimbia, kutembea na kufanya mazoezi katika maeneo yetu ya halmashauri zetu? (Makofi)

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, nimtoe tu wasiwasi Mheshimiwa Mbunge, hicho kinafanyika na ndiyo maana unaona kuna ushirikiano mkubwa wa Wizara ya Afya na Bunge, lakini na Wizara ya Michezo. Hata ukapoona tunapongojea michezo ya AFCON na mambo mengine utaona ushirikiano wa karibu sana na Wizara ya Afya, lakini pamoja na Wizara ya Michezo katika kuhakikisha tunafanya hayo. Sasa kwa sababu ni masuala ya kibajeti kila wakati tunaenda kitaifa, lakini pole pole mpaka tutashuka kwenye ngazi ya wilaya, lakini mambo hayo yanakwenda na yanaenda pamoja. (Makofi)

Name

Asia Abdulkarim Halamga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. BENARDETA K. MUSHASHU aliuliza:- Je, kuna mpango gani kuhakikisha sekta zote zinashiriki vita dhidi ya magonjwa yasiyoambukiza yanayosababisha vifo vingi nchini?

Supplementary Question 5

MHE. ASIA A. HALAMGA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana, je, ni upi mpango wa Serikali wa kupunguza gharama za matibabu ya figo kwenye kusafisha pamoja na upandikizaji kwa sababu ugonjwa huu kwa sasa umekuwa ukiwaathiri sana Watanzania na hasa walioko vijijini kwa sababu hawana uwezo wa kukidhi gharama za upandikizaji, lakini pia za usafishaji? (Makofi)

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, kweli kama anavyosema Mheshimiwa Mbunge kumekuwepo na gharama kubwa za kusafisha figo na mambo mengine siyo tu figo, lakini hata tiba mbalimbali ambazo zinatokana na haya magonjwa ya kuambukiza, lakini kama anakumbuka Mheshimiwa Mbunge miaka mitatu iliyopita kusafisha figo ilikuwa ni shilingi 400,000 mpaka shilingi 600,000 lakini kwa sasa utakuta baadhi ya hospitali zetu zimeanza utakuta zingine shilingi 120,000 na zingine shilingi 200,000. Maana yake zinaanza kushuka, lakini mpango wa Serikali ni nini?

Mheshimiwa Spika, moja; ni kuhakikisha vifaa ambavyo vinatumika kwenye kufanya shughuli hiyo, vitendanishi na dawa tuna access moja kwa moja viwandani, lakini pia kuhakikisha katika watu wanaongiza nchini hivyo vitu tunaongeza wadau mbalimbali wanaoingiza ili kutengeneza competition ya wafanyabiashara ili pia kushusha bei wakati MSD nayo inatengeneza mkakati wa kwenda viwandani na kuhakikisha inachuka yenyewe na ku-supply kwenye hospitali zetu ili kushusha gharama.