Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 26 Health and Social Welfare Wizara ya Afya 335 2025-05-16

Name

Bernadeta Kasabago Mushashu

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. BENARDETA K. MUSHASHU aliuliza:-

Je, kuna mpango gani kuhakikisha sekta zote zinashiriki vita dhidi ya magonjwa yasiyoambukiza yanayosababisha vifo vingi nchini?

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA alijibu:-

Mheshimiwa Spika, Serikali inatekeleza Mpango Mkakati wa Tatu wa Kitaifa wa Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa Yasiyoambukiza, 2021 – 2026 ambapo unajumuisha sekta zote na umeainisha mikakati mahsusi ya udhibiti wa visababishi vya magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo kuimarisha uratibu na ushirikishwaji wa sekta mtambuka, kuimarisha miundombinu ya utoaji wa huduma, kuwajengea uwezo watumishi katika kukabiliana na magonjwa yasiyoambukiza, kuimarisha na kusimamia shughuli za utafiti pamoja na kuhamasisha wananchi kuhusu njia za kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza. Njia hizi ni kufanya mazoezi pamoja na kuzingatia kanuni bora za lishe.

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha. (Makofi)