Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Aloyce John Kamamba
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kakonko
Primary Question
MHE. ALOYCE J. KAMAMBA aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kuwapandisha madaraja kwa mserereko walimu wenye changamoto ya kupandishwa madaraja wakiwemo walimu wa Kakonko?
Supplementary Question 1
MHE. ALOYCE J. KAMAMBA: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili madogo ya nyongeza.
Kwanza ninaishukuru sana Serikali kwa majibu, lakini nampongeza sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri ambayo anaendelea kuifanya hasa ya kuangalia watumishi na kuwapandisha vyeo na kuwalipa stahiki zao. (Makofi)
Swali la kwanza, wapo walimu walioajiriwa mwaka 2013 katika Wilaya ya Kakonko lakini hawakupandishwa madaraja kama walivyostahili. Nini kauli ya Serikali kuhsuiana na walimu hao ambao hawakuweza kupata madaraja yao kwa wakati?
Mheshimiwa Spika, swali la pili, ninayo orodha ya watumishi wa Wilaya ya Kakonko ambao walishawasilisha majina na maombi kwenye Ofisi ya Mheshimiwa Waziri, lakini hawajaweza kushughulikiwa, je, yupo tayari nimkabidhi orodha hiyo ili imsaidie katika kuhakikisha kwamba watumishi hao wanapata stahili zao?
Name
Deus Clement Sangu
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kwela
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwanza nimpongeze sana Mheshimiwa Mwalimu Aloyce Kamamba kwa kufuatilia stahiki za walimu na masuala yote yanayohusu walimu nchini.
Mheshimiwa Spika, nikijibu maswali yake mawili ya nyongeza kwamba kuna walimu mwaka 2013 walioajiriwa mwaka huo kwamba hawakupandishwa vyeo, ni kweli na siyo wote, mwaka 2013 kuna baadhi yao na katika zoezi hili tayari walimu wapatao 48,189 wameshapandishwa vyeo. Hata hivyo naomba nikuhakikishie Mheshimiwa Mbunge kuwa Serikali tayari imeshatoa waraka kuwataka Wakurugenzi wote wa Halmashauri wahakikishe kuwa kabla ya mwisho wa mwezi huu walete majina ya watumishi walisahaulika, na siyo walimu tu ni watumishi wote wa umma wanatakiwa kutufikishia taarifa zao ili kabla ya mwaka wa fedha kuisha tuwe tayari tumewapandisha madaraja kulingana na walivyostahili kuwa, lakini orodha hiyo ambayo Mheshimiwa Mbunge unayo nakukaribisha, utaileta ili tuweze kuifanyiakazi kwa kuwa tayari utakuwa umeturahisihia kazi ya kuleta na pia katika Manispaa ya Kigoma Ujiji changamoto hii ni kubwa. Nitoe rai pia kwa Mkurugenzi ahakikishe orodha hiyo anaileta kwa wakati.
Name
Sophia Hebron Mwakagenda
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ALOYCE J. KAMAMBA aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kuwapandisha madaraja kwa mserereko walimu wenye changamoto ya kupandishwa madaraja wakiwemo walimu wa Kakonko?
Supplementary Question 2
MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA: Mheshimiwa Spika, ahsante, katika mwongozo huo ambao mmeagiza wakurugenzi walete kwanza imechukua muda mrefu na walimu wengi pamoja na wafanyazi wengine waliojiendeleza wenyewe kielimu mmekataa kuwahamishia katika kile kipya walichokisomea ijapokuwa wamejilipia wenyewe.
Ni lini Serikali sasa mtaona umuhimu wa walimu waliojisomesha basi muwapandishe madaraja kwa kutumia kile walichokiongeza katika elimu yao?
Name
Deus Clement Sangu
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kwela
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Spika, ahsante na naomba kujibu swali la Mheshimiwa Sophia, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, ni kweli kuna baadhi ya walimu waliojiendeleza na sio kwamba Serikali imekataa kuwafanyia recategorization, hapana, ni kwamba waajiri wao hawajaleta taarifa hizo ili tuweze kuzifanyia kazi, kwa hiyo naomba pia niendelee kutoa maelekezo au nitoe rai kwa Wakurugenzi wote kama kuna walimu au watumishi wa aina hiyo walete hizo taarifa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumi wa Umma na Utawala Bora nao wataingia kwenye orodha hii kabla ya mwaka huu wa fedha watafanyiwa recategorization.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved