Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2020-2025 | Session 19 | Sitting 26 | Public Service Management | Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora) | 332 | 2025-05-16 |
Name
Aloyce John Kamamba
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kakonko
Primary Question
MHE. ALOYCE J. KAMAMBA aliuliza:-
Je, Serikali ina mpango gani wa kuwapandisha madaraja kwa mserereko walimu wenye changamoto ya kupandishwa madaraja wakiwemo walimu wa Kakonko?
Name
Deus Clement Sangu
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kwela
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA alijibu:-
Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa kifungu cha 6(1)(b) cha Sheria ya Utumishi wa Umma, Sura, 298 jukumu la kuwapandisha vyeo watumishi ni la mwajiri husika. Jukumu hili hutekekelezwa baada ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kutoa mwongozo kuwataka waajiri kuandaa na kuwasilisha ikama na bajeti ya mwaka husika wa fedha na Ofisi kuridhia utekekelezaji wa bajeti hiyo.
Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2024/2025 Serikali imetoa mwongozo unaohusu upandishwaji vyeo na ubadilishaji kada ikiwemo na kwa watumishi waliocheleweshwa kupandishwa vyeo. Hivyo, nitoe wito kwa waajiri wote nchini kutekeleza kwa wakati mwongozo huo ili kuepusha malalamiko kwa watumishi wa umma wenye changamoto za kupandishwa vyeo wakiwemo watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved