Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Oran Manase Njeza
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mbeya Vijijini
Primary Question
MHE. ORAN M. NJEZA K.n.y. MHE. MASACHE N. KASAKA aliuliza:- Je, lini Serikali itazipandisha hadhi Barabara ya Isenyela - Sangambi - Lupa - Lualaje na Chunya Godima - Sangambi kuwa chini ya TANROADS?
Supplementary Question 1
MHE. ORAN M. NJEZA: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana, kwa kuwa barabara hizo zimeharibika sana na mvua zinazoendelea Wilaya ya Chunya, je, ni lini Serikali itapeleka fedha kwa ajili ya kurekebisha barabara hizo?
Swali la pili, je, ni lini Serikali itazipandisha Barabara za Ruanda, Sapanda mpaka Msituni ziliopo Wilaya ya Mbeya Vijijini?
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Spika, wakati Serikali ikiwa inaendelea na taratibu ya kuzipandisha hadhi Barabara hizi za Isenyela - Sangambi - Lupa - Lualaje na Chunya Godima mpaka Sangambi, Serikali inaendelea kutenga fedha kwa ajili ya kuzikarabati barabara hizi. Kwa hiyo, katika mipango ya Serikali tayari kuna fedha ambazo zimetengwa kwa ajili za kuendelea kuzihudumia barabara hizi na pindi zitakapopandishwa hadhi kwenda katika hadhi ya mkoa na kuanza kuhudumiwa na TANROADS basi angalau kwa kipindi hicho zinakuwa tayari zinaendelea kuwasaidia wananchi.
Mheshimiwa Spika, kuhusiana na swali la pili, kama nilivyotangulia kujibu kwenye majibu ya msingi kwamba mchakato wa kupandisha hadhi barabara kutoka barabara za wilaya zenye hadhi za wilaya ambazo zinahudumiwa na TARURA kuzipeleka kwenye hadhi ya mkoa na sasa zitahudumiwa na TANROADS kuna mchakato ambao unaanzia katika Bodi ya Barabara ya Mkoa.
Kwa hiyo, naomba nimtaarifu Mheshimiwa Oran Njeza tutaanzisha mchakato huo katika ngazi ya kimkoa kwenye Bodi ya Barabara na kupeleka na kuwasilsiha mapendekezo kwenda kwa Waziri wa Ujenzi kwa ajili ya hatua ya kuweza kuzipandisha hadhi barabara alizozitaja Mheshimiwa Mbunge sasa kuanza kuhudumiwa na TANROADS na kuwa na hadhi za kimkoa.
Name
Saashisha Elinikyo Mafuwe
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Hai
Primary Question
MHE. ORAN M. NJEZA K.n.y. MHE. MASACHE N. KASAKA aliuliza:- Je, lini Serikali itazipandisha hadhi Barabara ya Isenyela - Sangambi - Lupa - Lualaje na Chunya Godima - Sangambi kuwa chini ya TANROADS?
Supplementary Question 2
MHE. SAASHISHA E. MAFUWE: Mheshimiwa Spika, ahsante, Kikao cha Barabara cha Mkoa wa Kilimanjaro kilishapitia hatua zote na kupendekeza barabara ambazo zinatakiwa kupandishwa hadhi; je, ni lini sasa Serikali itamalizia mchakato huo wa kupandisha barabara za Mkoa wa Kilimanjaro lakini zikiwemo za Wilaya ya Hai? (Makofi)
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Spika, ni kweli kabisa Bodi ya Barabara za Mkoa wa Kilimanjaro imefanya mchakato wa kuweza kubaini ni barabara zipi ambazo wanaona zinastahili sifa ya kuweza kupandishwa hadhi kutoka barabara za wilaya kuwa na hadhi ya barabara za mkoa na kama nilivyotangulia kujibu kwenye majibu ya msingi, kwamba baada ya Bodi ya Barabara kuwa imepitisha na imefanya mchanganuo na kuzibaini barabara hizi, basi mapendekezo yanawasilishwa Wizara ya Ujenzi na baada yah apo Wizara ya Ujenzi inaendelea na mchakato wa kuziidhinisha nakuzipandisha hadhi kuja sasa katika hadhi ya barabara za mkoa.
Kwa hiyo, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi tutaendelea kuwasiliana na wenzetu ili kuona wamefikia wapi katika hatua ya mwisho ambayo sasa ni ya kuidhinisha maombi ambayo yameletwa na Mkoa wa Kilimanjaro kwenye barabara hizi ambazo zitoke wilaya ziende katika ngazi ya mkoa.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved