Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Agnes Elias Hokororo

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. AGNES E. HOKORORO aliuliza:- Je, lini Serikali itatekeleza ahadi ya kukamilisha ujenzi wa Kituo cha Afya Namwanga baada ya Halmashauri ya Masasi kuanza ujenzi huo?

Supplementary Question 1

MHE. AGNES E. HOKORORO: Mheshimiwa Spika, ahsante, pamoja na majibu mazuri ya Serikali naomba kuuliza maswali madogo mawili za nyongeza.

Mheshimiwa Spika, kituo hicho kikikamilika kitawezesha kutoa huduma za afya katika kata nne ikiwemo Mpindimbi, Nanjota na Mijelejele; je, Serikali haioni haja ya kuharakisha mipango yake ili kuisadia halmashauri?

Swali la pili, Kijiji cha Chipingo kilichopo Kata ya Namwanga wananchi wake wanapata huduma mbali ambapo wanatembea zaidi za kilometa 60 na mwaka jana akina mama wawili walijifungulia darajani, je, Serikali imepanga kupeleka shilingi ngapi kusaidia juhudi za halmashauri katika ujenzi wa kituo hicho cha afya?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, ahsante sana, ni kweli kwamba Kituo cha Afya cha Namwanga ni kituo ambacho kitahudumia kata takribani nne zinazozunguka kituo hiki cha afya na ni kituo muhimu sana kwa wananchi wa Jimbo la Lulindi, Halmashauri ya Masasi Vijijini.

Mheshimiwa Spika, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Hokororo kwamba baada ya halmashauri kutenga fedha na ujenzi kuendelea, tayari Ofisi za Rais, TAMISEMI tumekiweka kwenye mpango wa Mfuko wa Dunia kwa maana ya World Bank kwa ajili ya kupeleka fedha mapema iwezekenanvyo kujenga majengo mengine yanayobaki ili kiweze kutoa huduma zote za msingi za kituo cha afya.

Mheshimiwa Spika, kuhusiana na zahanati hiyo, kwanza niwapongeze wananchi wa kijiji hicho kwa kuchangia nguvu zao kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho cha afya na niwahakikishie kwamba Serikali hii wa Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kipindi cha miaka minne imejenga na kukamilisha maboma ya zahanati zaidi ya 980 yakiwemo maboma katika Halmashauri ya Masasi.

Mheshimiwa Spika, niwahakikishie tu kwamba fedha zitapekewa kwa ajili ya kumalisha zahanati hiyo ili iweze kuanza kutoa huduma na kuondoa adha ya wananchi kusafiri umbali mrefu.

Name

Pauline Philipo Gekul

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Babati Mjini

Primary Question

MHE. AGNES E. HOKORORO aliuliza:- Je, lini Serikali itatekeleza ahadi ya kukamilisha ujenzi wa Kituo cha Afya Namwanga baada ya Halmashauri ya Masasi kuanza ujenzi huo?

Supplementary Question 2

MHE. PAULINE P. GEKUL: Mheshimiwa Spika, nikushukuru, ni lini Serikali itapeleka fedha kwa kukamilisha Vituo vya Afya Nangara na Singe? Singe ilikuwa ahadi ya Mheshimiwa Rais, ni lini fedha hizi zitafika?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, Kituo cha Afya cha Nangara tayari kimewekwa kwenye mpango wa Benki ya Dunia na Bahati njema Mheshimiwa Gekul tumewasiliana mara kadhaa, lakini pia tunafahamu Kituo cha Afya cha Singe ni ahadi ya Mheshimiwa Rais na kama ilivyo utaratibu wa ahadi za viongozi wakuu, ahadi za Mheshimiwa Rais ni kipaumbele namba moja katika utengaji wa fedha kwa ajili ujenzi wa vituo hivyo.

Kwa hiyo, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Gekul kwamba vituo vyote hivyo vya afya tayari tumeviweka kwenye kipaumbele na mpango wake ni kupata fedha mapema iwezekanavyo kwa ajili ya kuvijenga ili vianze kutoa huduma hizo kwa wananchi. (Makofi)

Name

Ritta Enespher Kabati

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Kilolo

Primary Question

MHE. AGNES E. HOKORORO aliuliza:- Je, lini Serikali itatekeleza ahadi ya kukamilisha ujenzi wa Kituo cha Afya Namwanga baada ya Halmashauri ya Masasi kuanza ujenzi huo?

Supplementary Question 3

MHE. DKT. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Spika, ahsante, lini Serikali itapeleka pesa katika Kata ya Ibumu iliopo katika Wilaya ya Kilolo kwa sababu wanatembea umbali mrefu sana kufuata matibabu zaidi ya kilometa 40 na hata Kata ya Mlafu jirani yao pia hawana kituo cha afya? Ahsante.

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, Serikali iliweka utaratibu wa kujenga vituo vya afya katika kata za kimkakati ambazo zinakidhi idadi ya watu wasiopungua 10,000 lakini zenye umbali mkubwa wa kutoka kwenye kituo cha jirani zaidi cha huduma za afya. kwa hiyo, ikiwa kituo hicho cha kata hiyo inayotajwa na Mheshimiwa Mbunge inakidhi vigezo hivyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba Ofisi ya Rais, TAMISEMI tutafanya mawasiliano na halmashauri ili tuanze kutenga fedha kwa awamu kwa ajili za ujenzi wa kituo hicho cha afya.