Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2020-2025 | Session 19 | Sitting 26 | Regional Administration and Local Government Authorities | Ofisi ya Rais TAMISEMI. | 330 | 2025-05-16 |
Name
Agnes Elias Hokororo
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. AGNES E. HOKORORO aliuliza:-
Je, lini Serikali itatekeleza ahadi ya kukamilisha ujenzi wa Kituo cha Afya Namwanga baada ya Halmashauri ya Masasi kuanza ujenzi huo?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:-
Mheshimiwa Spika, Kituo cha Afya Namwanga kinajengwa kwa fedha za mapato ya ndani ya Halmashauri ya Masasi ambapo kimeanza na ujenzi wa jengo la kuhudumia wagonjwa wa nje (OPD), mpaka sasa Halmashauri ya Masasi imetoa shilingi milioni 100 na ujenzi upo katika hatua ya ukamilishaji.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2025/2026 Serikali kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri ya Masasi imetenga shilingi milioni 50 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje (OPD) na Serikali Kuu itapeleka fedha za ujenzi wa majengo mengine katika Kituo cha Afya cha Namwanga, ahsante. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved