Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Asia Abdulkarim Halamga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ASIA A. HALAMGA K.n.y. MHE. CECILIA D. PARESSO aliuliza: - Je, Serikali ina mkakati gani wa kukabiliana na wanyama waharibifu na wakali wanaotoka Hifadhi ya Ngorongoro na Ziwa Manyara – Karatu?

Supplementary Question 1

MHE. ASIA A. HALAMGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili madogo ya nyongeza. Nitumie nafasi hii kuipongeza Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kuhakikisha kwamba inakuwa na mkakati mkubwa na endelevu wa kuweza kutatua changamoto zinazowakabili wananchi dhidi ya wanyama waharibifu. Je, ni lini sasa ujenzi huu fensi kilometa 15 utaanza? Kwa kuwa katika majibu ya msingi yalieleza kwamba ujenzi utanza kwenye bajeti hii ya mwaka huu, na kwa kuwa tuko mwezi wa Pili wa mwaka wa bajeti, na mwaka huu unapofika mwezi wa Sita mwaka wa bajeti unakuwa umekwisha, je, nini kauli ya Serikali, ituambie itaanza lini?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili. Je, Mheshimiwa Naibu Waziri yupo tayari kufuatana na Mheshimiwa Cecilia Daniel Paresso ili kwenda kujionea kadhia hiyo wanayopata wananchi wa Karatu? (Makofi)

Name

Hamad Hassan Chande

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kojani

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa nafasi ya kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Asia Halamga. Kwanza, nimpongeze sana kwa mashirikiano mazuri, na kwa kuwa ameonesha kabisa anauliza maswali ambayo yanaenda kujenga. Pia nimpongeze na Mwenyekiti ambaye kimsingi ndio ameuliza swali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nimwondoe shaka Mheshimiwa Asia kwamba ujenzi huu utafanyika ndani ya mwaka huu wa fedha haraka iwezekanavyo kwa sababu tayari fedha imeshaingia. Mradi wote gharama yake ni shilingi milioni 900, na tayari shilingi milioni 300 zimepelekwa site. Ninachomhakikishia ni kwamba wakati wowote, wala asihofu ya kwamba tumefika mwezi wa Pili, ujenzi unaenda kuanza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu swali lake la pili, huu ni wajibu. Ninaachaje sasa kufuatana na Mwenyekiti kupata baraka zake kwenda katika site hiyo huko? Ahsante sana. (Makofi)