Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Jesca David Kishoa
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. JESCA D. KISHOA aliuliza: - Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa Barabara ya Iguguno - Nduguti - Sibiti (kilometa 89) na Barabara unganishi za daraja la Mto Sibiti (kilometa 24.83)?
Supplementary Question 1
MHE. JESCA D. KISHOA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru, pamoja na majibu ya Serikali, lakini Wilaya ya Mkalama ndiyo Wilaya pekee katika Mkoa wa Singida, ambayo, ili ufike makao makuu ni lazima upigwe na vumbi la kutosha. Ninaomba, ili kuwaepusha wananchi na adha hii, kwa sababu shughuli za kijamii zinadorora na hata za kiuchumi, na wakati mwingine wananchi wa kule wanapoteza maisha, ninaomba commitment ya Serikali, very seriously, barabara hii inaanza kujengwa lini, kama ambavyo imekuwa ikiahidiwa mara zote?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, je, Serikali haioni kwamba kuna umuhimu sasa wa kupeleka fedha za kutosha kwenye maeneo ambayo yana geographical features zile ngumu, kama milima, mabonde na mito, kwa ajili ya wao kujenga miundombinu ya barabara, madaraja pamoja na ma-culvert, ili wananchi hawa waepukane na adha kutokana na hali waliyonayo ya kimazingira? Ninakushukuru sana.
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza, ninamhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba, kwa kutambua hilo, Serikali iliona pia kuna umuhimu wa kuanza mjini, pale Nduguti, tukiwa tunakuja Singida Mjini kuanzia Iguguno, lakini mpango ni kuijenga barabara yote kwa lami hadi kwenda Sibiti. Kwa hiyo, nakuhakikishia tumetangaza tenda, lakini mkandarasi akawa ame-tender juu. Kwa hiyo, tuko kwenye kuitangaza tena upya dhamira ipo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tulitangaza, lakini tukashindwana na mkandarasi kwa sababu, alikuwa ame-tender juu. Dhamira ni kubwa sana, tunaendelea kuitangaza na kuanza kuijenga muda siyo mrefu. Tupo kwenye utaratibu wa kuijenga. Hilo ni la kwanza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, kuhusu maeneo korofi, yenye mito na mabonde. Kama kuna kitu Tanzania tumefanya na katika Wizara ya Ujenzi ni pale ambapo Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hasa kutokana na changamoto tuliyoipata, alipoamua kutafuta fedha zaidi ya shilingi bilioni 500 kwa ajili ya kujenga madaraja na makalavati na maeneo yote yenye mabonde ambayo yalikuwa yanakwamisha, kupeleka hizo fedha. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, huu ni kati ya mradi mkubwa ambao wale ambao maeneo yao yamepitiwa, wanafahamu, tumejenga madaraja mengi, tumeondoa changamoto ya milima ambako ilikuwa inaporomoka, tumeijenga na tunaendelea kukamilisha. Mwisho wa mwezi huu ndiyo deadline, madaraja zaidi ya 81 yamejengwa. Pia mabonde mengi yamefanyika. Hatuwezi tukamaliza maeneo mengi, lakini maeneo yote korofi tumeyafanya na tutaendelea kufanya hivyo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kama kuna changamoto kubwa sana kwenye Jimbo lako Mheshimiwa tunakukaribisha, labda litakuwa halikuonekana, lakini hata Mkoa wa Singida mradi huo ulipita na tumejenga madaraja mengi sana. Ahsante. (Makofi)
Name
Festo Richard Sanga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Makete
Primary Question
MHE. JESCA D. KISHOA aliuliza: - Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa Barabara ya Iguguno - Nduguti - Sibiti (kilometa 89) na Barabara unganishi za daraja la Mto Sibiti (kilometa 24.83)?
Supplementary Question 2
MHE. FESTO R. SANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Naibu Waziri utakubaliana na mimi leo ni mara ya 13 ninauliza kuhusu barabara ya Makete - Mbeya. Ni takribani miaka minne toka mmesaini mkataba na hakuna hata sentimeta moja ya lami Jimbo la Makete.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia utakubaliana na mimi mkandarasi huyu certificate zime-mature tayari, lakini hamjamlipa, na zaidi, mimi kama Mbunge kwenye kazi ya Kibunge ya kuisemea barabara hii na kukuuliza maswali, nimefanya kazi yangu. Ipi ni kauli ya Serikali kwa wananchi wa Makete kuhusu barabara hii? (Makofi)
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninataka kumhakikishia Mheshimiwa Mbunge, barabara ya Makete – Isyonje ipo kwenye ujenzi, japo kwa sasa ni kweli kuna changamoto kubwa sana ya mvua inayonyesha. Ninakuhakikishia Mheshimiwa Mbunge, mtafute mkandarasi, tayari tumeshamlipa hizo certificate zake, ahsante. (Makofi)
Name
Zuberi Yahya Mfaume
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Morogoro Kusini
Primary Question
MHE. JESCA D. KISHOA aliuliza: - Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa Barabara ya Iguguno - Nduguti - Sibiti (kilometa 89) na Barabara unganishi za daraja la Mto Sibiti (kilometa 24.83)?
Supplementary Question 3
MHE. ZUBERI Y. MFAUME: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya wananchi wa Jimbo la Morogoro Kusini na wananchi wa Halmashauri ya Morogoro ningependa kujua, ni lini ujenzi wa barabara ya Bigwa – Kisaki utaanza? Ahsante. (Makofi)
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, Bigwa – Kisaki, kilomita 78, mkandarasi ameshalipwa na ameshaanza kazi za awali kufanya site clearance ikiwa ni pamoja na kujenga zile kambi za mhandisi mshauri. Kwa hiyo, kazi imeshaanza Bigwa – Kisaki. Ahsante. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved