Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 2 | Sitting 6 | Works and Transport | Wizara ya Ujenzi | 99 | 2026-02-03 |
Name
Jesca David Kishoa
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. JESCA D. KISHOA aliuliza: -
Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa Barabara ya Iguguno - Nduguti - Sibiti (kilometa 89) na Barabara unganishi za daraja la Mto Sibiti (kilometa 24.83)?
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imeanza mipango ya ujenzi wa Barabara ya Iguguno – Nduguti – Sibiti yenye urefu wa kilometa 84.95 ambapo upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa barabara hii umekamilika. Ili kurahisisha utekelezaji wa mradi huu, Serikali imepanga kuijenga kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa barabara unganishi za Daraja la Mto Sibiti, Mkandarasi amepatikana, na taratibu za kuanza kazi za ujenzi zinaendelea. Aidha, Serikali inaendelea na taratibu za manunuzi ya kumpata mkandarasi, kwa ajili ya ujenzi wa Sehemu ya Nduguti Mjini yenye urefu wa kilometa 10. Baada ya hatua za manunuzi kukamilika na mkandarasi kupatikana, kazi za ujenzi zitaanza, ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved