Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Suma Ikenda Fyandomo
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ESTER A. BULAYA K.n.y. MHE. PATRICK A. MWALUNENGE aliuliza: - Je, lini Serikali itakamilisha Mradi mkubwa wa Maji kutoka chanzo cha Mto Kiwira ili kukomesha tatizo la maji Mbeya Mjini?
Supplementary Question 1
MHE. SUMA I. FYANDOMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru sana kwa kunipa nafasi hiyo. Hili swali linahusu wananchi wa Mkoa wa Mbeya. Ninashukuru sana kwa majibu ya Serikali. Huo Mradi wa Mbeya unasubiriwa na kutegemewa sana na wananchi. Nimekuwa nikiulizia mara nyingi sana hapa, ninategemea sana mimi pamoja na wananchi wa Mkoa wa Mbeya kwamba majibu hayo yatakuwa ni sahihi na watakwenda kupata mradi huo wa maji.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la nyongeza. Kwa kuwa mradi wa maji ambao ni mkubwa sana kwenye Wilaya ya Kyela unategemewa sana, lakini mpaka sasa hivi haujakamilika, je, tenki hilo litakamilika lini? Ahsante.
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan inaendelea kutekeleza miradi mbalimbali nchini, na katika awamu iliyopita, zaidi ya miradi 3,714 yenye gharama ya shilingi trilioni 1.8 imekamilika, na sasa tunayo miradi 778 yenye gharama ya shilingi trilioni 1.3 inaendelea kutekelezwa ukiwemo mradi wa Kyela kama ambavyo Mheshimiwa Mbunge ameeleza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kikubwa nitaelekeza mamlaka husika wanaosimamia mradi huu kuhakikisha kwamba wanashirikiana na mkandarasi ili mradi huu uweze kukamilika kwa wakati, lakini pia Serikali tutaendelea kupeleka fedha kwa ajili ya mkandarasi kutokwama kwa namna yoyote ile ili lengo ni kwamba, wananchi wa Mkoa wa Mbeya na Kyela waweze kupata huduma ya majisafi na salama.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sasa Mkoa wa Mbeya upatikanaji wa maji ni zaidi ya 90% na miradi inayoendelea ni zaidi ya shilingi bilioni 128 katika Mkoa wa Mbeya. Nakushukuru sana. (Makofi)
Name
Mwita Mwikwabe Waitara
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tarime Vijijini
Primary Question
MHE. ESTER A. BULAYA K.n.y. MHE. PATRICK A. MWALUNENGE aliuliza: - Je, lini Serikali itakamilisha Mradi mkubwa wa Maji kutoka chanzo cha Mto Kiwira ili kukomesha tatizo la maji Mbeya Mjini?
Supplementary Question 2
MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushuruku sana. Kwa kuwa sasa hivi Wizara ya Maji ina mitambo ya kuchimba visima, na kuna kata kama zile za Pemba, Mbogi, Gwitiryo na maeneo mengine hayana maji. Ni lini Serikali itapeleka wataalam wakatafiti kwenye vijiji katika Jimbo la Tarime Vijijini ili pale yanapopatikana maji chini ya ardhi watu wapate maji ya kunywa? Ahsante.
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi Wizara ya Maji tunampongeza sana, na kumshukuru sana Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Baada ya kununua mitambo ya kuchimba maji ndani ya kipindi cha miaka mitatu, tumeweza kuchimba visima 1,956. Hii ni rekodi ambayo haijawahi kutokea tangu tulivyoanza kuchimba visima 1,930 pale Mtukula.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa Mheshimiwa Mbunge tutapeleka wataalamu wetu wa bonde, wataenda kufanya utafiti na baada ya hapo mitambo yetu ambayo ilinunuliwa na Serikali ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan wataenda kutekeleza mradi huo ili wananchi wa Mheshimiwa Mbunge waweze kupata huduma ya majisafi na salama.
Name
Dickson Nathan Lutevele
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mafinga Mjini
Primary Question
MHE. ESTER A. BULAYA K.n.y. MHE. PATRICK A. MWALUNENGE aliuliza: - Je, lini Serikali itakamilisha Mradi mkubwa wa Maji kutoka chanzo cha Mto Kiwira ili kukomesha tatizo la maji Mbeya Mjini?
Supplementary Question 3
MHE. DICKSON N. LUTEVELE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru kwa kupata nafasi ya kuuliza swali. Kwanza kabisa niishukuru Serikali kwamba Halmashauri ya Mji wa Mafinga ni moja kati ya miji ambayo ilipata Mradi wa Maji wa Miji 28 na mradi huu ilikuwa ukamilike mwezi Juni mwaka uliopita, lakini mpaka sasa hivi mradi huu uko 28% tu ya utekelezaji wake. Ninaomba kauli ya Serikali, je, ni lini mradi huu utakamilika ili wananchi wa Mafinga waweze kupata maji? (Makofi)
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nimpongeze sana kaka yangu Mwenezi wa Wilaya na Mbunge wa Jimbo hilo ambaye ameanza kwa kasi kubwa sana, na mwezi mmoja tu uliopita nilikuwa naye kwenye ziara katika jimbo lake, na tulipitia baadhi ya miradi, na mradi ambao ameuongelea ni mradi unaotekelezwa na Jandu Plumbers ambapo ni kweli ulikuwa unasuasua, lakini tuliwaita wakandarasi tukakaa tukakubaliana warudi site waweze kuendelea kutekeleza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa tunaamini kwamba kwa kadiri fedha ambavyo zitakuwa zinapatikana tutahakikisha tunamwezesha mkandarasi aweze kukamilisha huu mradi kwa wakati. Ninashukuru sana.
Name
Devotha Daniel Mburarugaba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ESTER A. BULAYA K.n.y. MHE. PATRICK A. MWALUNENGE aliuliza: - Je, lini Serikali itakamilisha Mradi mkubwa wa Maji kutoka chanzo cha Mto Kiwira ili kukomesha tatizo la maji Mbeya Mjini?
Supplementary Question 4
MHE. DEVOTHA D. MBURARUGABA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi. Ni lini Wilaya ya Kyerwa itaweza kupata maji ya uhakika? Kwani mradi ambao uko Wilaya ya Kyerwa unatekelezwa kwa kusuasua. Nilitaka kujua shida ni mkandarasi au kuna mkakati mwingine?
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kabisa kuna baadhi ya miradi ambayo inaendelea kutekelezwa lakini kuna mingine ambayo inasuasua. Nimwelekeze RM Mkoa wa Kagera aende Kyerwa leo akafanye tathmini na kujiridhisha kuna changamoto gani, ili atuletee kwa ajili ya kuchukua hatua stahiki kulingana na uzembe ambao unaweza ukasababishwa na wakandarasi, na kama siyo mkandarasi, tujue kwamba tatizo liko wapi?
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru sana.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved