Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 2 | Sitting 6 | Water and Irrigation | Wizara ya Maji | 93 | 2026-02-03 |
Name
Patrick Adkin Mwalunenge
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mbeya Mjini
Primary Question
MHE. ESTER A. BULAYA K.n.y. MHE. PATRICK A. MWALUNENGE aliuliza: -
Je, lini Serikali itakamilisha Mradi mkubwa wa Maji kutoka chanzo cha Mto Kiwira ili kukomesha tatizo la maji Mbeya Mjini?
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Maji, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Patrick Mwalunenge, Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inaendelea na utekelezaji wa mradi wa kutoa maji Mto Kiwira kwenda Jijini Mbeya. Miongoni mwa kazi zinazotekelezwa kupitia mradi huo ni pamoja na ujenzi wa dakio (intake) na mtambo wa kutibu maji lita milioni 117 kwa siku, ujenzi wa matanki mawili yenye uwezo wa kuhifadhi maji lita milioni 10 sambamba na ulazaji wa mabomba umbali wa kilometa 37.
Mheshimiwa Mwenyekiti, utekelezaji wa mradi huo umefikia wastani wa 48% na kwa mujibu wa mkataba unatarajiwa kukamilika mwezi Disemba, 2026 ambapo utanufaisha zaidi ya wakazi 890,000 wa Jiji la Mbeya na Mji wa Mbalizi. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved