Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Boniphace Mwita Getere
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bunda
Primary Question
MHE. BONIPHACE M. GETERE aliuliza:- Je, lini Wananchi walioharibiwa mazao yao na Tembo katika Vijiji vya Jimbo la Bunda watalipwa kifuta jasho?
Supplementary Question 1
MHE. BONIPHACE M. GETERE: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru. Pamoja na majibu mazuri ya Serikali ninayo maswali mawili.
Mheshimiwa Spika, swali la kwanza. Kwa kuwa wananchi wa vijiji vya Hunyari, Kihumbu, Mariwanda, Sarakwa, Mugeta, Kyandege, Tingirima, Nyangere na Kambugo wameahidiwa kulipwa toka mwezi wa Novemba, je, Serikali kwa siku za karibuni sasa, ni lini watalipwa fedha zao? (Makofi)
Mheshimiwa Spika, swali la pili. Naibu Waziri amezungumza vizuri kwamba sasa wameleta mfumo mpya wa kuwalipa watu kupitia akaunti zao za benki na kwenye simu. Wanajua katika nchi yetu tuna matatizo ya NIDA? Mtu anaweza kusajili watu wawili, watatu. Sasa huo mfumo wa kwenda kuwalipa watu kwa kutumia mtindo wa zamani, wako tayari kwenda kuelimisha watu juu ya jambo hilo? Ahsante.
Name
Hamad Hassan Chande
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kojani
Answer
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, swali lake la kwanza, ninaomba nimtoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba wakati wowote kuanzia sasa, kwa sababu mchakato umeshakamilika, wananchi waliopata madhara hayo wataenda kulipwa stahiki yao. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, swali lake la pili, kama nilivyojibu katika swali la msingi kwamba pamoja na mfumo wetu mpya tulionao wa kisasa tunaenda kurejea mfumo ule wa zamani wa kufika uwandani kuwalipa wananchi stahiki zao na kabla ya kuwalipa tutaendelea kutoa elimu kama ambavyo Mheshimiwa Mbunge amependekeza. Ahsante sana. (Makofi)
Name
Mary Daniel Surati
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Serengeti
Primary Question
MHE. BONIPHACE M. GETERE aliuliza:- Je, lini Wananchi walioharibiwa mazao yao na Tembo katika Vijiji vya Jimbo la Bunda watalipwa kifuta jasho?
Supplementary Question 2
MHE. MARY D. SURATI: Mheshimiwa Spika, ninamshukuru Naibu Waziri kwa majibu mazuri ambayo ameendelea kuyatoa. Pia nilikuwa ninaomba wananchi wa Jimbo la Seregenti wanaomba kufahamu, ni lini Serikali itaanza kutoa fidia stahiki inayoendana na hasara wanazopata wananchi wanaoathirika na Wanyamapori? (Makofi)
Name
Hamad Hassan Chande
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kojani
Answer
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, Serikali inatoa fidia stahiki kwa mujibu wa sheria na kanuni zilizowekwa. Kwa hiyo, ninamhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba wananchi hawa wataendelea kupata fidia ambazo wanastahiki, na kwa sasa hakuna mtu yeyote ambaye atakosa haki yake ya msingi.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved