Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 2 Sitting 2 Natural Resources and Tourism Wizara ya Maliasili na Utalii 36 2026-01-28

Name

Boniphace Mwita Getere

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bunda

Primary Question

MHE. BONIPHACE M. GETERE aliuliza:-

Je, lini Wananchi walioharibiwa mazao yao na Tembo katika Vijiji vya Jimbo la Bunda watalipwa kifuta jasho?

Name

Hamad Hassan Chande

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kojani

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha 2024/2025 Wizara ililipa kifuta jasho na machozi jumla ya shilingi 311,160,000 kwa wananchi 1,115 wa Wilaya ya Bunda. Aidha, Wizara imekamilisha uchambuzi wa madai ya kifuta jasho na machozi ambapo shilingi 524,122,500 kwa wananchi 1,603 wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda zitalipwa. Kwa sasa Wizara inakamilisha taratibu za malipo hayo ili wananchi husika walipwe stahiki zao kwa mujibu wa Kanuni kupitia mfumo wa kieletroniki ujulikanao kwa jina la Problem Animal Information System – (PAIS).

Mheshimiwa Spika, sambamba na mfumo huu mpya kwa sasa, Serikali itaendelea kulipa wananchi ambao hawana account au namba za siku kwa kutumia utaratibu wa awali ambapo wataalamu hufika uwandani kufanya malipo hayo. Ahsante sana.