Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Tarimba Gulam Abbas

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kinondoni

Primary Question

MHE. TARIMBA G. ABBAS aliuliza:- Je, Serikali haioni haja ya kuweka Sharti la Kisheria la Watoto wakubwa kutunza wazazi wao wasiojiweza?

Supplementary Question 1

MHE. TARIMBA G. ABBAS: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru kwa kunipa nafasi. Ninamshukuru Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu yake. Wajibu wa kisheria wa kuwalea wazazi kwa maana ya wazazi wasio na uwezo katika nchi nyingine wanaita Filial Responsibility Laws, maana yake ni kwamba hizi sheria siyo ngeni.

Mheshimiwa Spika, je, Serikali haioni haja ya kwenda kupata uzoefu kwenye nchi ambazo zina sheria kama hizi ili kuzileta nchi zikatumika kwa minajili ya kusaidia wazazi wetu?

SPIKA: Mheshimiwa Tarimba, twende kwenye swali.

MHE. TARIMBA G. ABBAS: Mheshimiwa Spika, swali la pili, sioni kama kuna mizania. Zipo sheria zinazolazimisha wazazi kulea watoto wao, lakini hakuna sheria zinazolazimisha watoto kuwalea wazazi.

Mheshimiwa Spika, ninaomba nimwulize Waziri, haoni kwamba kuna uharaka sasa wa kuleta hiyo sheria Bungeni ili tuweze tukaijadili? Ninakushukuru sana. (Makofi)

Name

Maryprisca Winfred Mahundi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM: Mheshimiwa Spika, napenda kumshukuru sana Mheshimiwa Tarimba Abbas kwa maswali mazuri ya kujenga. Kama nilivyoweza kujielekeza kwenye jibu langu la msingi, nianze kujibu hapa umuhimu wa kwenda kujifunza, tuko tayari na tunafanya hivyo.

Mheshimiwa Spika, Wizara yetu inatembea nchi mbalimbali kuendelea kujifunza. Vilevile hii sera ambayo tumeirekebisha mwaka 2024 tukiizingatia ina majibu sahihi kwa nchi yetu na jamii kuona umuhimu wa vijana wetu kulea wazee wao wasiojiweza.

Mheshimiwa Spika, vilevile, uharaka wa kuleta jambo hili Bungeni, tutaendelea kuona mchakato uliopo wa wadau kukusanya maoni, na kuona namna njema ya kuhakikisha wazee hawa wanaendelea kupatiwa matunzo.

Mheshimiwa Spika, vilevile kwenye sera yetu tumeelekeza namna wazee hawa pia tunawashirikisha. Hivyo, nipende tu kusema tutaendelea kukusanya maoni kwa wadau pamoja na Bunge letu Tukufu. Tutaendelea kuomba ushirikiano wenu kuhakikisha wazee wote wanapata matunzo kwa sababu wao ni tunu, wamefanya mengi kwenye nchi, wanastahili heshima na matunzo salama. (Makofi)